Likoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Likoni
Nchi Kenya
Kaunti Mombasa
Likoni.
Feri ya Likoni.

Likoni ni sehemu ya mji wa Mombasa nchini Kenya katika kaunti ya Mombasa.

Likoni iko barani ikitazama upande wa kusini wa kisiwa cha Mombasa. Ni mahali pa feri inayounganisha kisiwa cha Mombasa na bara upande wa kusini. Upande huo hakuna daraja kwa sababu mkono wa bahari ni pia mdomo wa bandari ya Kilindini na meli kubwa hupita kila saa. Kwa sababu hiyo daraja lingehitaji kuwa kubwa mno na hadi sasa serikali imekosa pesa ya kujenga daraja kubwa namna hiyo.

Kampuni ya Feri ya Likoni iko na mashua nne zinazovusha abiria kwa miguu na magari mfululizo. Njia hii inatumiwa na watu pamoja na magari mengi yanayoelekea sehemu mbalimbali za kusini mwa pwani kama vile Kwale, Diani na hata nchi jirani ya Tanzania.