Leo mfiadini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kifodini cha Danieli na wenzake.

Leo Somma wa Corigliano Calabro alikuwa mmojawapo kati ya wenzi wa Danieli Fasanella waliofia dini huko Ceuta (Afrika Kaskazini) tarehe 10 Oktoba 1227. Walikuwa Ndugu Wadogo wamisionari huko Moroko.[1]Wote walikuwa mapadri isipokuwa Donulus.

Walitangazwa watakatifu na Papa Leo X mwaka 1516.

Sikukuu yao inaadhimishwa kila tarehe 10 Oktoba.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kifodini cha Berardo wa Carbio na wenzake kilichotokea Moroko mwaka 1219 kilifanya Wafransisko wengi watamani kufuata nyayo zao kwa kuhubiri Injili kwa wasio Wakristo.

Basi, mwaka 1227, uilofuata ule wa kifo cha mwanzilishi, Fransisko wa Asizi, watawa 6 wa kanda ya Toscana, Agnelus, Samueli, Donulus, Leo mwenyewe, Hugolino na Nikola wa Sassoferrato, walimuomba Elia wa Cortona, mkuu wa shirika, awaruhusu kwenda Moroko kuwahubiria Waislamu.

Kisha kukubaliwa, walikwenda Hispania, alipojiunga nao kama kiongozi Danieli Fasanella wa Belvedere, mkuu wa kanda ya Calabria.

Toka huko walivuka bahari na tarehe 20 Septemba walishukia Afrika, walipobaki siku chache katika kijiji kilichokaliwa hasa na wafanyabiashara Wakristo.

Halafu, Jumapili asubuhi, waliingia mjini Ceuta, wakaanza mara kuhubiri kwa kupinga Uislamu. Kwa sababu hiyo walipekelekwa kwa sultani ambaye, akiwadhani ni vichaa, aliagiza watiwe gerezani. Walibaki humo hadi Jumapili iliyofuata, ambapo sultani kwa mabembelezo na vitisho alijaribu kuwafanya wakane dini yao.

Aliposhindwa, aliagiza wauawe. Kila mmojawao alimkaribia Danieli ili kupata baraka yake na ruhusa ya kumfia Yesu. Wote walikatwa kichwa.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Father Candide Chalippe (1 June 2007). The Life and Legends of Saint Francis of Assisi. Echo Library. pp. 164–. ISBN 978-1-4068-4456-6. Retrieved 8 July 2013. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.