Berardo mfiadini
Mandhari
Berardo (alizaliwa Carbio, Umbria, Italia, karne ya 12) akafia dini ya Ukristo kwa kuchomwa kwa upanga huko Marakesh, leo nchini Morocco pamoja na Ndugu Wadogo wenzake Petro wa San Gemini, Oto, mapadri kama yeye, Akursius na Adiutus, mabradha.
Ndio Wafransisko wafiadini wa kwanza. Aliposikia habari zao, Fransisko wa Asizi alishangilia, "Sasa kweli naweza kusema nina Ndugu Wadogo watano". Ndiye aliyekuwa amewatuma kumhubiri Kristo kwa Waislamu, nao wakafanya hivyo kwanza Sevilia, Hispania, hadi walipofukuzwa kwenda Moroko.
Wote wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu, hasa tangu mwaka 1481 walipotangazwa na Papa Sixtus IV.
Sikukuu yao ni tarehe 16 Januari[1], siku ya kifodini chao mwaka 1220.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- (Kiitalia) Santi Berardo, Otone, Pietro, Accursio e Adiuto Protomartiri dell’Ordine dei Frati Minori
- (Kijerumani) Antonius von Padua Ilihifadhiwa 9 Mei 2003 kwenye Wayback Machine. - mentioned in the entry for Saint Anthony
- Catholic Encyclopedia article