Adiutus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Berardo na wenzake.

Adiutus alizaliwa Italia ya kati, akafia dini ya Ukristo huko Morocco pamoja na Ndugu Wadogo wenzake Berardo, Petro wa San Gemini, Oto na Akursius.

Ndio Wafransisko wafiadini wa kwanza. Aliposikia habari zao, Fransisko wa Asizi alishangilia, "Sasa kweli naweza kusema nina Ndugu Wadogo watano".

Wote wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu, hasa tangu mwaka 1481 walipotangazwa na Papa Sixtus IV.

Sikukuu yao ni tarehe 16 Januari, siku ya kifodini chao mwaka 1220.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]