Nenda kwa yaliyomo

Petro wa San Gemini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Watakatifu Berardo na wenzake.

Pietro wa San Gemini alizaliwa katika kijiji hicho cha Italia ya kati, akafia dini ya Ukristo huko Morocco pamoja na Ndugu Wadogo wenzake Berardo, Oto, Akursius na Adiutus.

Ndio Wafransisko wafiadini wa kwanza. Aliposikia habari zao, Fransisko wa Asizi alishangilia, "Sasa kweli naweza kusema nina Ndugu Wadogo watano". Ndiye aliyekuwa amewatuma kumhubiri Kristo kwa Waislamu, nao wakafanya hivyo kwanza Sevilia, Hispania, hadi walipofukuzwa kwenda Moroko.

Wote wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu, hasa tangu mwaka 1481 walipotangazwa na Papa Sixtus IV.

Sikukuu yao ni tarehe 16 Januari, siku ya kifodini chao mwaka 1220.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.