Nenda kwa yaliyomo

Akursius wa Aguzzo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Akursius)
Berardo na wenzake.

Akursius wa Aguzzo alizaliwa Italia ya Kati, akafia dini ya Ukristo huko Moroko pamoja na Ndugu Wadogo wenzake Berardo wa Carbio, Petro wa San Gemini, Oto wa Stroncone na Adiutus wa Narni.

Ndio Wafransisko wafiadini wa kwanza. Aliposikia habari zao, Fransisko wa Asizi alishangilia, "Sasa kweli naweza kusema nina Ndugu Wadogo watano". Ndiye aliyekuwa amewatuma kumhubiri Kristo kwa Waislamu, nao wakafanya hivyo kwanza Sevilia, Hispania, hadi walipofukuzwa kwenda Moroko.

Wote wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu, hasa tangu mwaka 1481 walipotangazwa na Papa Sixtus IV.

Sikukuu yao ni tarehe 16 Januari, siku ya kifodini chao mwaka 1220.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Marejeo ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk 21
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 419-421

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.