Nenda kwa yaliyomo

Lauryn Hill

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lauryn Hill
Lauryn Hill akiimba mjini Ottawa mnamo 2012
Lauryn Hill akiimba mjini Ottawa mnamo 2012
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Lauryn Noel Hill
Amezaliwa 26 Mei 1975 (1975-05-26) (umri 49)
Asili yake East Orange, New Jersey, Marekani
Aina ya muziki hip hop, underground hip hop, alternative hip hop, soul, neo-soul, R&B, reggae, muziki wa asili, acoustic
Kazi yake Mwimbaji, rapa, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi, mwigizaji
Ala Sauti, gitaa, piano
Miaka ya kazi 1993-hadi leo
Studio Columbia, Ruffhouse
Ame/Wameshirikiana na The Fugees, Mary J Blige, Talib Kweli,Aretha Franklin
Tovuti Lauryn-Hill
Lauryn Noel Hill

Lauryn Noel Hill (amezaliwa tar. 26 Mei 1975) ni mshindi mara nane wa Tuzo za Grammy akiwa kama mwimbaji, rapa, mwanamuziki, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi za muziki, na mwigizaji bora wa filamu kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Lauryn Hill. Katika shughuli zake za awali, alianza kujibebea sifa kubwa katika ulimwengu wa muziki wa hip hop akiwa kama mwanamke pekee wa kundi la muziki huo la The Fugees.

Mnamo 25 Agosti katika mwaka wa 1998, akaanza kufanya kazi kama msanii wa kujitegemea na kuweza kutoa albamu moja iliyompatia mafanikio makuwa kabisa. Albamu ilikwenda kwa jina la The Miseducation of Lauryn Hill, albamu iliyosaidia kuinua muziki wa neo-soul katika ngazi za kibiashara.

Baada ya miaka minne ya mapumziko, akatoa albamu ya MTV Unplugged No. 2.0 iliyorekodiwa mnamo 21 Julai 2001 katika studio za MTV. Hill ameshinda tuzo nane za Grammy na pia ni mama wa watoto watano aliozaa na Rohan Marley, mtoto wa nne wa mwanamuziki wa raggae wa zamani - Bob Marley.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Lauryn Hill alizaliwa mnamo tar. 26 Mei ya mwaka wa 1975, katika mji wa East Orange, New Jersey. Hill alikuwa mtoto wa pili kuzaliwa na mwalimu wa Kiingereza - Valerie Hill na mwekaji programu za kompyuta Mal Hill. Akiwa mtoto, Hill alikuwa akisiliza rekodi nyingi muziki wa soul uliokuwa unafanywa na wazazi wake na studio za Motown zile za miaka ya 1960.

Muziki huo ulikuwa karibu kidogo na nyumbani kwa kina Hill. Mal Hill alikuwa akiimba nyimbo katika maharusi, Valerie alikuwa akipiga piano, na kaka mkubwa wa Lauryn Melaney alikuwa akipiga saxophone, gitaa, ngoma, harmonica, zeze, na piano.

Hill alianza kazi za uimbaji wakiwa na umri mdogo sana. Mnamo mwaka 1988 akiwa na umri mwa miaka 13, Hill alianza kuonekana katika maonyesho ya usiku akiwa kama mwimbaji kujitolea wa katika maonyesho ya It's Showtime at the Apollo.[1][2][3]

Albamu zake

[hariri | hariri chanzo]
Maelezo ya albamu
The Miseducation of Lauryn Hill
TBA

Single zake

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Jina Chart positions Albamu
U.S. U.S. R&B U.S. Rap UK
1998 "Can't Take My Eyes Off You" 351 45 The Miseducation of Lauryn Hill
"Deep In My Heart"²
"Doo Wop (That Thing)" 1 2 1 3
1999 "Lost Ones" 271
"Ex-Factor" 21 7 4
"Everything Is Everything" 35 14 19
"To Zion" 77
"Nothing Even Matters"
(akimshirikisha D'Angelo)
105³ 25

Single alizoshirikishwa na baadhi ya vibwagizo

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Jina Chart positions Albamu
U.S. U.S. R&B U.S. Rap UK
1996 "If I Ruled the World (Imagine That)"
(Nas akimshirikisha Lauryn Hill)
53 15 17 12 It Was Written
1997 "The Sweetest Thing" 18 Love Jones (kibwagizo)
"All My Time"
(Paid & Live akimshirikisha Lauryn Hill)
57 All My Time
"Turn Your Lights Down Low"
(with Bob Marley)
86 49 15 Chant Down Babylon
2002 "Mr. Intentional" MTV Unplugged No. 2.0
2005 "So High"
(John Legend akimshirikisha Lauryn Hill)
105³ 53 118 Get Lifted
2006 "Say"
(Method Man akimshirikisha Lauryn Hill)
66 4:21... the Day After
2007 "Lose Myself" Surf's Up Soundtrack

Mwonekano wake katika nyimbo nyingine

[hariri | hariri chanzo]
  1. "BRAFF: 'LAURYN HILL WAS MY COKE AND PEPSI PARTNER'". PR-inside.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-03-04. Iliwekwa mnamo 6 Septemba. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= (help); Unknown parameter |accessyear= ignored (|access-date= suggested) (help)
  2. Géraldine Khawly family tree
  3. "Rolling Stone: The Mystery of Lauryn Hill". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-08-17. Iliwekwa mnamo 2008-09-09. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: