Ready or Not
“Ready or Not” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya The Fugees kutoka katika albamu ya The Score | |||||
Imetolewa | 2 Septemba 1996 | ||||
Muundo | CD single, 12" single | ||||
Imerekodiwa | 1995 | ||||
Aina | Hip hop | ||||
Urefu | 3:47 | ||||
Studio | Ruffhouse Records | ||||
Mtunzi | Nelust Wyclef Jean Samuel Prakazrel Michel Lauryn Hill William Hart Thom Bell | ||||
Mtayarishaji | Wyclef, Lauryn Hill, Prakazrel "Pras" (co-producer), Jerry 'Wonder' Duplessis (co-producer) | ||||
Mwenendo wa single za The Fugees | |||||
|
"Ready or Not" ni single ya pili kutoka kwa kundi zima la muziki wa hip hop The Fugees. Wimbo ulitoka mwaka wa 1996 kutoka katika albamu ya The Score. Wimbo umechukua sampuli ya wimbo wa "Boadicea" wa Enya, na kiitikio chake kinatokana na wimbo wa "Ready or Not Here I Come (Can't Hide from Love)" wa The Delfonics. Wimbo ulitumia majuma mawili kwenye chati za UK Singles Chart mnamo mwezi wa Septemba katika mwaka wa 1996.[1]
Mwimbaji Enya alipanga kulishtaki kundi hili kwa sababu za ukiukwaji wa hakimiliki, kwa sababu hajaruhusu kundi la The Fugees kuchukua sampuli ya wimbo wake wa "Boadicea", kutoka katika albamu ya mwaka wa 1992, The Celts.[2] Hatimaye mpango mzima ukasawazishwa huko mahakamani.
Wimbo ulikuja kurudiwa tena na msanii wa muziki wa house wa Ulaya The Course mnamo mwaka wa 1997. Ulifikia nafasi ya #5 nchini Uingereza kwa mwezi wa Aprili katika mwaka huo.[3]
Rais wa Marekani Barack Obama ameuita "Ready or Not" kama wimbo wake kipenzi kutoka katika orodha ya 10 bora iliyotolewa na Blender mnamo mwezoi wa Agosti katika mwaka wa 2008.[4]
Orodha ya nyimbo
[hariri | hariri chanzo]CD1
[hariri | hariri chanzo]- "Ready Or Not" (Radio Version) - 3:47
- "Ready Or Not" (Salaam's Ready For The Show Remix) - 4:24
- "Ready Or Not" (Handel's Yaard Vibe Mix) - 4:41
- "The Score" - 4:32
CD2
[hariri | hariri chanzo]- "Ready Or Not" (Album Version) - 3:50
- "How Many Mics" - 4:23
- "Freestyle" - 5:03
- "Blame It On The Sun" - 5:41
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ The Fugees UK chart info Chartstats.com. Retrieved 23 Mei 2009.
- ↑ "Irish Voice article at archive.org". 1997-02-18. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2005-04-07. Iliwekwa mnamo 2007-03-26.
- ↑ The Course UK chart info Chartstats.com. Retrieved 23 Mei 2009.
- ↑ "White House DJ Battle". Blender Magazine. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-04-27. Iliwekwa mnamo 2008-08-04.