Lauryn Hill
Lauryn Hill | |
---|---|
Lauryn Hill akiimba mjini Ottawa mnamo 2012
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Lauryn Noel Hill |
Amezaliwa | 26 Mei 1975 |
Asili yake | East Orange, New Jersey, Marekani |
Aina ya muziki | hip hop, underground hip hop, alternative hip hop, soul, neo-soul, R&B, reggae, muziki wa asili, acoustic |
Kazi yake | Mwimbaji, rapa, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi, mwigizaji |
Ala | Sauti, gitaa, piano |
Miaka ya kazi | 1993-hadi leo |
Studio | Columbia, Ruffhouse |
Ame/Wameshirikiana na | The Fugees, Mary J Blige, Talib Kweli,Aretha Franklin |
Tovuti | Lauryn-Hill |
Lauryn Noel Hill (amezaliwa tar. 26 Mei 1975) ni mshindi mara nane wa Tuzo za Grammy akiwa kama mwimbaji, rapa, mwanamuziki, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi za muziki, na mwigizaji bora wa filamu kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Lauryn Hill. Katika shughuli zake za awali, alianza kujibebea sifa kubwa katika ulimwengu wa muziki wa hip hop akiwa kama mwanamke pekee wa kundi la muziki huo la The Fugees.
Mnamo 25 Agosti katika mwaka wa 1998, akaanza kufanya kazi kama msanii wa kujitegemea na kuweza kutoa albamu moja iliyompatia mafanikio makuwa kabisa. Albamu ilikwenda kwa jina la The Miseducation of Lauryn Hill, albamu iliyosaidia kuinua muziki wa neo-soul katika ngazi za kibiashara.
Baada ya miaka minne ya mapumziko, akatoa albamu ya MTV Unplugged No. 2.0 iliyorekodiwa mnamo 21 Julai 2001 katika studio za MTV. Hill ameshinda tuzo nane za Grammy na pia ni mama wa watoto watano aliozaa na Rohan Marley, mtoto wa nne wa mwanamuziki wa raggae wa zamani - Bob Marley.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Lauryn Hill alizaliwa mnamo tar. 26 Mei ya mwaka wa 1975, katika mji wa East Orange, New Jersey. Hill alikuwa mtoto wa pili kuzaliwa na mwalimu wa Kiingereza - Valerie Hill na mwekaji programu za kompyuta Mal Hill. Akiwa mtoto, Hill alikuwa akisiliza rekodi nyingi muziki wa soul uliokuwa unafanywa na wazazi wake na studio za Motown zile za miaka ya 1960.
Muziki huo ulikuwa karibu kidogo na nyumbani kwa kina Hill. Mal Hill alikuwa akiimba nyimbo katika maharusi, Valerie alikuwa akipiga piano, na kaka mkubwa wa Lauryn Melaney alikuwa akipiga saxophone, gitaa, ngoma, harmonica, zeze, na piano.
Hill alianza kazi za uimbaji wakiwa na umri mdogo sana. Mnamo mwaka 1988 akiwa na umri mwa miaka 13, Hill alianza kuonekana katika maonyesho ya usiku akiwa kama mwimbaji kujitolea wa katika maonyesho ya It's Showtime at the Apollo.[1][2][3]
Muziki
[hariri | hariri chanzo]Albamu zake
[hariri | hariri chanzo]Maelezo ya albamu |
---|
The Miseducation of Lauryn Hill
|
TBA
|
Single zake
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Jina | Chart positions | Albamu | |||
---|---|---|---|---|---|---|
U.S. | U.S. R&B | U.S. Rap | UK | |||
1998 | "Can't Take My Eyes Off You" | 351 | 45 | — | — | The Miseducation of Lauryn Hill |
"Deep In My Heart"² | — | — | — | — | ||
"Doo Wop (That Thing)" | 1 | 2 | 1 | 3 | ||
1999 | "Lost Ones" | 271 | — | — | — | |
"Ex-Factor" | 21 | 7 | — | 4 | ||
"Everything Is Everything" | 35 | 14 | — | 19 | ||
"To Zion" | — | 77 | — | — | ||
"Nothing Even Matters" (akimshirikisha D'Angelo) |
105³ | 25 | — | — |
Single alizoshirikishwa na baadhi ya vibwagizo
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Jina | Chart positions | Albamu | |||
---|---|---|---|---|---|---|
U.S. | U.S. R&B | U.S. Rap | UK | |||
1996 | "If I Ruled the World (Imagine That)" (Nas akimshirikisha Lauryn Hill) |
53 | 15 | 17 | 12 | It Was Written |
1997 | "The Sweetest Thing" | — | — | — | 18 | Love Jones (kibwagizo) |
"All My Time" (Paid & Live akimshirikisha Lauryn Hill) |
— | — | — | 57 | All My Time | |
"Turn Your Lights Down Low" (with Bob Marley) |
86 | 49 | — | 15 | Chant Down Babylon | |
2002 | "Mr. Intentional" | — | — | — | — | MTV Unplugged No. 2.0 |
2005 | "So High" (John Legend akimshirikisha Lauryn Hill) |
105³ | 53 | — | 118 | Get Lifted |
2006 | "Say" (Method Man akimshirikisha Lauryn Hill) |
— | 66 | — | — | 4:21... the Day After |
2007 | "Lose Myself" | — | — | — | — | Surf's Up Soundtrack |
Mwonekano wake katika nyimbo nyingine
[hariri | hariri chanzo]- 1996: "Stay Gold" (kutoka katikaYoung Zee albamu yaMusical Meltdown (Promo LP))
- 1996: "If I Ruled the World" (kutoka katikaNas albamu yaIt Was Written)
- 1997: "Retrospective For Life" (kutoka katikaCommon albamu yaOne Day It'll All Make Sense)
- 1998: "On That Day" (kutoka katikaCeCe Winans albamu yaEverlasting Love)
- 1998: "A Rose Is Still A Rose" (kutoka katikaAretha Franklin albamu yaA Rose Is Still a Rose)
- 1999: "All That I Can Say" (kutoka katikaMary J. Blige albamu ya"Mary (album)"
- 1999: "Turn Your Lights Down Low" kutoka katikaBob Marley tribute albamu yaChant Down Babylon)
- 1999: "Do You Like The Way" (kutoka katika Carlos Santana albamu yaSupernatural)
- 2002: "Selah" (from Divine Secrets of the Ya-Ya Sisterhood Soundtrack)
- 2004: "The Passion" (from The Passion of the Christ: Songs)
- 2005: "So High (Cloud 9 Remix) (kutoka katikaJohn Legend kutolewa kawa albamu ya"Get Lifted")
- 2007: "Music" (kutoka katikaJoss Stone albamu yaIntroducing Joss Stone)
- 2007: "Lose Myself" (kutoka katikaSurf's Up kibwagizo)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "BRAFF: 'LAURYN HILL WAS MY COKE AND PEPSI PARTNER'". PR-inside.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-03-04. Iliwekwa mnamo 6 Septemba.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
(help); Unknown parameter|accessyear=
ignored (|access-date=
suggested) (help) - ↑ Géraldine Khawly family tree
- ↑ "Rolling Stone: The Mystery of Lauryn Hill". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-08-17. Iliwekwa mnamo 2008-09-09.
{{cite web}}
: Unknown parameter|=
ignored (help)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Official site
- Lauryn Hill's personal website
- Januari 2006: Interview with Essence magazine 2005: They Call Me Ms. Hill Ilihifadhiwa 8 Septemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- Juni 2005: Lauryn Hill Def Poetry Jam Performance
- 30 Oktoba 2003: Rolling Stone magazine Ilihifadhiwa 17 Agosti 2008 kwenye Wayback Machine., "The Mystery of Lauryn Hill: She made one of the greatest albums of the Nineties—then what happened?" by Touré