Kipanya-misitu
Mandhari
Kipanya-misitu | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 21:
|
Vipanya-misitu ni wanyama wagugunaji wa jenasi Hylomyscus katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae ambao wanatokea katika misitu na maeneo yenye midambi ya Afrika kusini kwa Sahara.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Vipanya hawa wana masikio makubwa yenye mviringo na mkia mrefu na mwembamba. Urefu wa mwili ni mm 55-120, urefu wa mkia ni mm 75-175 na uzito ni g 6-42. Manyoya yao ni laini na kahawia hadi kahawianyekundu mgongoni na kijivu iliofifia tumboni.
Hukiakia usiku na wanaishi kwenye miti. Hula matunda, mbegu na wadudu.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Hylomyscus aeta, Kipanya-milia wa Uganda (Beaded wood mouse) – Burundi, Uganda
- Hylomyscus alleni (Allen's wood mouse)
- Hylomyscus anselli, Kipanya-misitu wa Ansell (Ansell's wood mouse) – Tanzania
- Hylomyscus arcimontensis, Kipanya-misitu wa Tao la Mashariki (Arc Mountain wood mouse) – Tanzania
- Hylomyscus baeri (Baer's wood mouse)
- Hylomyscus carillus (Angolan wood mouse)
- Hylomyscus denniae, Kipanya-misitu wa Ruwenzori (Montane wood mouse) – Uganda
- Hylomyscus endorobae, Kipanya-misitu Miguu-midogo (Small-footed wood mouse) – Kenya
- Hylomyscus grandis (Mount Oku wood mouse)
- Hylomyscus heinrichorum (Heinrich's wood mouse)
- Hylomyscus kerbispeterhansi, Kipanya-misitu wa Ml. Elgon (Kerbis Peterhans's wood mouse) – Kenya, Uganda
- Hylomyscus mpungamachagorum, Kipanya-misitu wa Mahale (Mahale wood mouse)
- Hylomyscus pamfi (Pamfi wood mouse)
- Hylomyscus parvus (Little wood mouse)
- Hylomyscus pygmaeus (Pygmy wood mouse)
- Hylomyscus simus (Flat-nosed wood mouse)
- Hylomyscus stanleyi, Kipanya-misitu wa Stanley (Stanley's wood mouse)
- Hylomyscus stella, Kipanya-misitu wa Stella (Stella wood mouse) – Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda
- Hylomyscus thornesmithae (Mother Ellen's wood mouse)
- Hylomyscus vulcanorum, Kipanya-misitu wa Volkano (Volcano wood mouse) – Burundi, Rwanda, Uganda
- Hylomyscus walterverheyeni (Walter Verheyen's mouse)