Kipanya-misitu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Hylomyscus)
Kipanya-misitu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Nusuoda: Myomorpha (Wanyama kama panya)
Familia: Muridae (Wanyama walio na mnasaba na panya)
Nusufamilia: Murinae (Wanyama wanaofanan na vipanya-miiba)
Jenasi: Hylomyscus
Thomas, 1926
Ngazi za chini

Spishi 21:

Vipanya-misitu ni wanyama wagugunaji wa jenasi Hylomyscus katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae ambao wanatokea katika misitu na maeneo yenye midambi ya Afrika kusini kwa Sahara.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Vipanya hawa wana masikio makubwa yenye mviringo na mkia mrefu na mwembamba. Urefu wa mwili ni mm 55-120, urefu wa mkia ni mm 75-175 na uzito ni g 6-42. Manyoya yao ni laini na kahawia hadi kahawianyekundu mgongoni na kijivu iliofifia tumboni.

Hukiakia usiku na wanaishi kwenye miti. Hula matunda, mbegu na wadudu.

Spishi[hariri | hariri chanzo]