Nenda kwa yaliyomo

Kijiwe cha nyongo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kijiwe cha nyongo
Mwainisho na taarifa za nje
Matamshi
Kundi MaalumuUpasuaji huku mwili mzima ukiwa umetiwa ganzi
DaliliHakuna, maumivu makali katika sehemu ya juu kulia ya tumbo[1][2][3]
Miaka ya kawaida inapoanzaBaada ya miaka 40[1]
Sababu za hatariTembe za kupanga uzazi, ujauzito, historia ya familia, unene wa kupita kiasi, kisukari, ugonjwa wa ini, kupunguza uzani kwa haraka[1]
Njia ya kuitambua hali hiiKulingana na dalili, zilizothibitishwa kupitia kupitia kipimo cha picha kinachotumia mawimbi ya sauti (ultrasound)[1][3]
KingaKuwa na uzani wa kiafya, lishe iliyo na vyakula vya nyuzinyuzi nyingi, lishe yenye kiwango cha chini cha kabohidrati[1]
MatibabuIsiyokuwa na dalili (Asymptomatic): hakuna[1]
Yenye maumivu: upasuaji[1]
Utabiri wa kutokea kwakeHali huwa sawa baada ya upasuaji[1]
Idadi ya utokeaji wakeasilimia 10-15% ya watu wazima (nchi zilizoendelea)[3]

Kijiwe cha nyongo (kwa Kiingereza: gallstone) ni kijiwe kinachoundika ndani ya kifuko cha nyongo kutokana na dutu zilizomo ndani ya nyongo.[1]

Neno cholelithiasis linaweza kumaanisha uwepo wa vijiwe vya nyongo au ugonjwa wowote unaosababishwa na vijiwe vya nyongo.[4] Watu wengi walio na vijiwe vya nyongo (karibia asilimia 80) kamwe hawana dalili.[1][2] Hata hivyo, ikiwa kijiwe cha nyongo kitaziba mrija wa nyongo, maumivu kama ya kukakamaa katika sehemu ya juu ya kulia ya tumbo, yanayojulikana kama shambulio la kifuko cha nyongo (biliary colic) yanaweza kutokea.[3] Hii hutokea kwa asilimia 1-4 ya watu walio na vijiwe vya nyongo kila mwaka.[3] Matatizo ya vijiwe vya nyongo yanaweza kujumuisha kuvimba kwa kifuko cha nyongo (cholecystitis), kuvimba kwa kongosho (pancreatitis), homa ya nyongo ya manjano na maambukizo ya mrija wa nyongo (cholangitis).[3][5] Dalili za matatizo hayo zinaweza kujumuisha maumivu yanayodumu zaidi ya saa tano, homa, ngozi ya manjano, kutapika, mkojo mweusi, na kinyesi kilichopauka.[1]

Sababu za hatari zinazochangia kuwa na vijiwe vya nyongo ni pamoja na tembe za kudhibiti uzazi, ujauzito, historia ya familia kuwa na vijiwe vya nyongo, unene wa kupindukia, kisukari, ugonjwa wa ini, au kupoteza uzani kwa haraka.[1] Dutu za nyongo zinazotengeneza vijiwe vya nyongo ni pamoja na kolesteroli, chumvi za nyongo na bilirubini.[1] Vijiwe vya nyongo vilivyotokana hasa na kolesteroli huitwa vijiwe vya kolesteroli na vile vinavyotokana hasa na bilirubini huitwa vijiwe vyenye rangi.[1][2] Vijiwe vya nyongo vinaweza kushukiwa kulingana na dalili.[3] Kisha utambuzi kwa kawaida huthibitishwa kupitia kipimo cha picha kinachotumia mawimbi ya sauti (ultrasound).[1] Matatizo yanaweza kugunduliwa kutumia vipimo vya damu.[1]

Hatari ya vijiwe vya nyongo inaweza kupunguzwa kwa kudumisha uzani wa kiafya kwa kufanya Mazoezi ya mwili na lishe yenye afya.[1] Ikiwa hakuna dalili, matibabu kwa kawaida hayahitajiki.[1] Kwa wale ambao wanakumbwa na mashambulizi ya kifuko cha nyongo, upasuaji wa kuondoa kifuko hicho hupendekezwa.[1] Upasuaji huo unaweza kufanywa kupitia chale kadhaa ndogo au kwa chale moja kubwa, kwa kawaida mtu akiwa ametiwa ganzi mwili wote.[1] Katika matukio ya nadra wakati upasuaji hauwezekani, dawa zinaweza kutumika kuondoa vijiwe hivyo au tiba ya kuvunjavunja vijiwe hivyo bila upasuaji (lithotripsy).[6]

Katika nchi zilizoendelea, asilimia 10-15 ya watu wazima wana vijiwe vya nyongo[3], lakini viwango katika sehemu nyingi za Afrika viko chini ya hadi asilimia 3.[7] Magonjwa yanayoshambulia na kifuko cha nyongo na mrija wa nyongo yalitokea kwa takriban watu milioni 104 (asilimia 1.6 ya watu) mwaka wa 2013 na kusababisha vifo 106,000.[8][9] Wanawake huathiriwa na ugonjwa huu zaidi kuliko wanaume na hutokea mara nyingi zaidi baada ya umri wa miaka 40.[1] Makabila fulani huwa na vijiwe vya nyongo mara nyingi zaidi kuliko mengine.[1] Kwa mfano, asilimia 48 ya Wamarekani Wenyeji wana vijiwe vya nyongo.[1] Mara baada ya kibofu cha nyongo kuondolewa, matokeo kwa ujumla huwa mazuri.[1]

  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 1.13 1.14 1.15 1.16 1.17 1.18 1.19 1.20 1.21 1.22 1.23 "Gallstones". NIDDK. Novemba 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Julai 2016. Iliwekwa mnamo 27 Julai 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 Lee, JY; Keane, MG; Pereira, S (Juni 2015). "Diagnosis and treatment of gallstone disease". The Practitioner. 259 (1783): 15–9, 2. PMID 26455113.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 3.5 3.6 3.7 Ansaloni, L (2016). "2016 WSES guidelines on acute calculous cholecystitis". World Journal of Emergency Surgery : WJES. 11: 25. doi:10.1186/s13017-016-0082-5. PMC 4908702. PMID 27307785.{{cite journal}}: CS1 maint: unflagged free DOI (link)
  4. Internal Clinical Guidelines Team (Oktoba 2014). "Gallstone Disease: Diagnosis and Management of Cholelithiasis, Cholecystitis and Choledocholithiasis. Clinical Guideline 188". Gallstone Disease: Diagnosis and Management of Cholelithiasis, Cholecystitis and Choledocholithiasis: 101. PMID 25473723.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Complications". nhs.uk. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Mei 2018. Iliwekwa mnamo 13 Mei 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Treatment for Gallstones". National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. Novemba 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-04-23. Iliwekwa mnamo 2018-06-06.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. editors, Ronnie A. Rosenthal, Michael E. Zenilman, Mark R. Katlic (2011). Principles and practice of geriatric surgery (tol. la 2nd). Berlin: Springer. uk. 944. ISBN 9781441969996. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-15. {{cite book}}: |last= has generic name (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  8. Global Burden of Disease Study 2013, Collaborators (22 Agosti 2015). "Global, regional, and national incidence, prevalence, and years lived with disability for 301 acute and chronic diseases and injuries in 188 countries, 1990-2013: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2013". Lancet. 386 (9995): 743–800. doi:10.1016/s0140-6736(15)60692-4. PMC 4561509. PMID 26063472. {{cite journal}}: |first= has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link)
  9. GBD 2013 Mortality and Causes of Death, Collaborators (10 Januari 2015). "Global, regional, and national age-sex specific all-cause and cause-specific mortality for 240 causes of death, 1990-2013: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2013". Lancet. 385 (9963): 117–71. doi:10.1016/s0140-6736(14)61682-2. PMC 4340604. PMID 25530442. {{cite journal}}: |first= has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link)