Kasimir Mtakatifu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Kasimir.

Mtakatifu Kasimir (kwa Kipolandi Kazimierz; Krakow, Poland, 3 Oktoba 1458 - Grodno, Belarus, 4 Machi 1484) alikuwa mwana wa mfalme wa Poland.

Ametambuliwa na Kanisa Katoliki chini ya Papa Adrian VI kuwa mtakatifu kuanzia mwaka 1522.

Tarehe ya kifo chake, yaani 4 Machi, ni pia sikukuu yake[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Katika maisha yake alidhihirisha fadhila za Kikristo, hasa usafi wa moyo, toba na upendo kwa maskini[2].

Alikuwa na imani thabiti, na aliheshimu sana Ekaristi na Bikira Maria.

Alifariki dunia mapema kwa ugonjwa wa Tibii mwaka 1484.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1296
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.