Joyce Msuya
Amezaliwa | 2 Januari 1968 Dar es Salaam |
---|---|
Nchi | Tanzania |
Kazi yake | Mtaalamu wa mazingira |
Joyce Msuya (alizaliwa Dar es Salaam, 2 Januari 1968) ni mwanabiolojia na mtaalamu wa mazingira kutoka Tanzania, aliyekuwa Katibu Mkuu Msaidizi wa UM kwa Shughuli ya Hisani na mratibu msaidizi wa miradi ya misaada ya hisani ya Umoja wa Mataifa.[1].
Hadi kuteuliwa kwa kazi hiyo Desemba 2021 alikuwa Kaimu Mkurugenzi Tekelezi wa Mradi wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Mazingira (UNEP) na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa UM tangu mwaka 2018.[2].
Maisha na elimu
[hariri | hariri chanzo]Joyce Msuya ni mtoto wa nne wa Cleopa Msuya aliyekuwa Katibu wa Wizara ya Uchumi na Mipango akaendelea kuhudumia kama Waziri Mkuu wa Tanzania mara tatu.
Alianza masomo kwenye shule ya msingi ya Forodhani, Dar es Salaam akamaliza Form VI Shule ya Sekondari ya Weruweru kwenye mkoa wa Kilimanjaro[3].
Alisoma Chuo Kikuu cha Strathclyde, Glasgow (Uskoti) alipopokea mwaka 1992 shahada ya kwanza katika somo la biokemia. Akaendelea na masomo yake Chuo Kikuu cha Ottawa, Kanada alipohitimu mwaka 1996 kwa shahada ya uzamili ya mikrobiolojia na elimu ya kingamaradhi[4].
Ameolewa na Onesmo Mpanju akazaa watoto wawili.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kumaliza masomo Msuya alikuwa na ajira za muda mfupi hadi kuajiriwa na Benki ya Dunia kwenye mwaka 1998[5] alipoendelea hadi mwaka 2018 katika nafasi mbalimbali, pamoja na kuwa mwakilishi wa benki katika Jamhuri ya Korea.
Kwenye Agosti 2018 alihamia ofisi kuu ya Umoja wa Mataifa akipewa nafasi ya Naibu Mkurugenzi Tekelezi wa UNEP. Baada ya kujiuzulu kwa Mkurugenzi Tekelezi Erik Solheim[6] kwenye Novemba 2018 amekuwa kaimu mkurugenzi tekelezi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Tanzania’s Joyce Msuya appointed UN Assistant Secretary-General for Humanitarian Affairs Archived 15 Desemba 2021 at the Wayback Machine., gazeti la Citizen 15-12-2021
- ↑ Joyce Msuya, tovuti ya UNEP, iliangaliwa Desemba 2021
- ↑ Hayo na mengine kutoka makala "Itachukua muda, fedha nyingi Dar es Salaam kuwa jiji la kisasa", katika gazeti la Mwananchi, tar 28 Machi 2019, uk. 13
- ↑ Joyce Msuya, tovuti ya UNEP, iliangaliwa 28 Machi 2019
- ↑ Joyce Msuya, tovuti ya UNEP, iliangaliwa 28 Machi 2019
- ↑ Mtanzania Joyce Msuya ateuliwa kaimu kiongozi wa shirika la UNEP lenye makao yake Nairobi, tovuti ya BBC-Swahili ya 21 Novemba 2018, iliangaliwa 28 Machi 2019
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Joyce Msuya kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |