Mradi wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Mazingira

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Bendera ya UNEP.

Mradi wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Mazingira (UNEP) ni mojawapo ya mashirika ya UM yaliyo chini ya jukumu la Baraza la Kiuchumi na Kijamii, yaani ECOSOC [1]. Mradi huu una kazi ya kuanzisha na kuendeleza miradi ya kuihifadhi mazingira ya binadamu jinsi ilivyo na hatimaye kuiboresha. Kwa kufanya hivi, UNEP inaonelea kuwa sote tuna jukumu la kuihifadhi na kuboresha mazingira ka vizazi zijazo. Makao makuu yapo mjini Nairobi.

Historia[hariri | hariri chanzo]

UNEP ulianzishwa na Baraza Kuu wa Umoja wa Mataifa mnamo tarehe 15 Desemba 1972 kupitia sheria la ishirini na saba. Mkurugenzi wa UNEP anajulikana kama mkurugenzi-tekelezi. Kwa sasa ni Bw. Achim Steiner alieichukua wahdhifu hiyo tarehe15 Machi,2006 kutoka kwa Bw. Klaus Toepfer aliyejiuzulu baada ya miaka minane katika wadhifu huo. UNEP imejuhusisha na mpango wa Kyoto kupunguza gesi zinazoongeza joto duniani.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]