Jini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Jini ni jina la Kiswahili lililotokana na jina la Kiarabu "Jin".

Majini ni viumbe wanaosadikika kuishi katika mazingira ya kila aina; pia baadhi ya watu wanaamini majini ni viumbe wenye uwezo mkubwa wa kufanya vitu tofautitofauti, pia wenye uwezo wa kujibadilisha kuwa katika hali waipendayo.

Kwa asilimia kubwa wenye imani ya uwepo wa mijini wanasema kuwa ni viumbe wasioweza kuonekana, hivyo imekuwa vigumu kupata uthibitisho wa moja kwa moja kuhusiana na viumbe hao.

Imani hiyo ilitangulia mwanzo wa Uislamu ikaingia dini hiyo na kwa njia hiyo kuenea katika nchi mbalimbali.

Kadiri yake majini waliumbwa na Mungu kwa kutumia moto na wakiwa wa jinsia mbili.

Ukristo haupatani na imani hiyo.

Lakini kuna madhehebu ya kikristo uamini uwepo wa majini na majini ni sawa na mashetani sema wenye kufuata mila za kiarabu.

Katika uislamu uamini kuwa kuna majini wazuri na majini wabaya kwa maana ya madhala yao katika maisha ya mwanadamu na waislamu wengine ufuga majini hao katika nyumba zao au miili yao na kuwafanya viumbe hawa kama wasaidizi au walinzi wa maisha yao kwa wale ambao uamini ni majini wazuri lakini wengine utumia majini waitwao wabaya kuharibu na kutesa maisha ya watu wengine kwa kuwatuma kuwaingia miilini na kuleta magonjwa, kuharibu kazi au biashara ya mtu na hata familia.

Lakini wakristo uamini kuwa hakuna jini mzuri bali wote ni wabaya na wao na mashetani ni sawa hivyo ni adui wa mkristo yeyote yule kama alivyo Shetani. Wakristo wamekuwa wakifanya maombi kwa watu ambao wanateswa na majini hawa ili kuwafungua kutoka katika nguvu zao za uovu, majini katika ukristo ni sawa na mapepo ambao Bwana Yesu (mwanzilishi wa ukristo) aliwatoa miilini mwa watu na kuwapa mamlaka na uwezo wanafunzi wake (wafuasi wake ambao ni wakristo leo) kuwatoa pia.

Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jini kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.