Japhet Ngailonga Hasunga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Japhet Ngaionga Hasunga


Aliingia ofisini 
7 October 2017

Aliingia ofisini 
November 2015

tarehe ya kuzaliwa (amezaliwa 23 Novemba
utaifa Mtanzanaia
chama CCM
mhitimu wa www.msm.nl (MBA)


Japhet Ngailonga Hasunga (alizaliwa 23 Novemba 1965) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha Chama Cha Mapinduzi (CCM). Alichaguliwa kuwa mbunge wa Vwawa kwa uchaguzi uliofanyika mwaka 2015 hadi mwaka 2020. [1] Ameoa na ana familia yake na miongoni mwa vitu anavyoviamini tangu utoto wake ni kule kuishi maisha ya kawaida na ndiyo maana anafanikiwa kujua mambo mengi ambayo yanamsaidia katika utenda kazi wake wa kazi za kila siku hasa kwa nafasi yake ya naibu waziri wa Maliasii na utalii kwani hukutana na makundi mengi mbalimbali na ni mongoni mwa watu wanao amini kwamba Asali ni mojawapo rasilimali nzuri ikitumiwa vizuri inaweza kukuza kukuza na kuendeleza utengamano kwa jamii lakini pia kukuza kuinua Uchumi wa nchi.[2]

Maisha/Kuzaliwa[hariri | hariri chanzo]

Japhet alizaliwa katika kijiji cha Iyula Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya ambapo wazazi wake waliishi hapo, alilelewa hapo hapo kijijini na kukulia hapo mpaka ilipofika wakati wa kupelekwa shule na aliishi maisha ya kawaida kama mtu mwingine na mwandishi wa ukurasa huu elezi alipo taka kujua kipi anakipenda tangu akiwa mtoto na ambacho anadhani kuwa anaendelea nacho hadi leo japo alianza kwa kicheko lakini mwisho wa yote alisema yeye alikuwa anapenda sana kujifunza kwa maana ya kutafuta elimu lakini anasema alikuwa na bidii ya kazi na mpaka leo yeye humshangaa sana mtu asiyependa kazi. Kama haitoshi mwandishi huyu katika kumfuatlia aligundua mahojia ya Japhet Ngailonga Hasunga na chombo kimoja cha habari alisisitiza jamii kupenda kazi hiyo ilikuwa ni tarehe 24 Novemba 20008.[3]

Maisha na Elimu[hariri | hariri chanzo]

Japhet Ngailonga Hasunga mapema mwaka 1976 mpaka 1982 ndio mwaka ambao pengine ulitengeneza njia ya kusaka elimu, kwani mwaka huo ndio alipata nafasi ya kusonga mbele kwa kuwa na alama za juu zilizo mpekea kujiunga na Shule ya Sekondari ya Sangu iliyopo Mbozi, Mbeya kwa wakati huo sasa ni Songwe na huo ulikuwa ni mwaka 1982 hadi 1986 alipofanikiwa kupata cheti cha Elimu ya kawaida ya Sekondari (CSEE). Kuanzia mwaka 1987 mpaka 1989 ambapo alijiunga na Shule ya Sekondari ya Mzumbe na kuhitimu elimu ya juu ya Secondari kwa kuzawadiwa cheti cha (ACSEE), kati ya mwaka 1992 mpaka 1995 alijiunga na chuo cha Maendeleo ya manajimenti Mzumbe (IDM) na kupata Stashahada ya Juu ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu. Mwaka 1998 alihitimu Shahada ya juu ya Uhasibu na Ukaguzi wa Mahesabu (CPA) kutoka NBAA na kusajiliwa kama Mhasibu kamili Mwaka 2001. Mnamo mwaka 2006 hadi 2007 Hasunga alisoma katika chuo cha Manejimenti cha Maastrichs nchini Uholanzi na kutunukiwa Shahada ya udhamili katika masuala ya Biashara, sera za Uchumi na mikakati. (MBA)

Harakati za Maisha na Siasa[hariri | hariri chanzo]

Japhet Ngailonga Hasunga alianza harakati za kisiasa mnamo mwaka aipojunga na chma cha NCCR–Mageuzi na kuajiliwa kama mtendaji wa shughuli za chama, wakati huo chama kilikuwa katika hatua za kujiimalisha na hivyo kubahatika kuwa miongoni mwa wanachama waanzilishi wa NCCR–Mageuzi, hiyo ikiwa ni mwaka 1992 hapo bado chamaa kilikuwa hakijasajiliwa na hakika unapotaja mafanikio ya NCCR–Mageuzi ni lazima pia uzungumzie utumishi wa Japhet Ngailonga Hasunga kama mwanamageuzi harisi. Katika kipindi hicho yeye alikuwa ni Afisa Utawala wa chama, mwaka huohuo (1992) akawa miongoni mwa wanachama waanzilishi. Kwa hiyo wakati NCCR–Mageuzi ikipata usaji wake Tarehe 21 March 1993 yeye alikuwa ni mtu muhimu katka ukuzi wa chama. Mwaka 1994 alichaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza Kuu, Mwaka 1995 alichaguwa kuwa Naibu Mkurugenzi idara ya sera na nyaraka, pia katika mwaka huohuo wa 1995 alibahatika kuwa Kaimu Naibu Katibu wa Cham. kiu yake yakuwa katika Chama kikubwa cha siasa ilitimia mwaka 2001 alipojiunga na Chama cha Mapinduzi ambacho ni chama tawala na utaona mara baada ya kujiunga na CCM aliendelea na harakati zake za kujiongezea elimu. Na viongozi wa chama katika kumuona kwamba anatosha kuwa miongoni mwa wawakilishi wa wananchi kupitia Chama cha Mapinduzi akapewa dhamana ya kupeperusha bendera ya Chama katika uchaguzi mkuu wa 2015 kwa nafasi ya ubunge akiwakilisha Jimbo la Uchaguzi a Vwawa katika Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya kwa wakati huo, sasa hivi Wilaya ya Mbozi ipo katika Mkoa wa Songwe katika mgawanyo wa kawaida wa maeneo ya kiutawala. Hasunga katika uchaguzi huo aliibuka kidedea kwa kumshinda mpinzani wake kwa zaidi ya kura 36,705 dhidi ya kura 35,400 za mpinzani wake kwa hiyo ilikuwa ni tofauti ya kura 1305 hii ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa uchaguzi jimbo la Mbozi.[4]Japhet Ngailonga Hasunga anabainisha kwamba wananchi kwa sasa wamebaini kwamba kumbe hawakufanya makosa kwa kumpa kura kwani mnamo tarehe 9 october 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alimwamini na kumpa dhamana ya kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Maliasili na Utalii ambayo anaitumikia hadi leo. Lakini jingine ambalo limpa nafasi ya kurudi kwa wananchi ni namna ambavyo serikali ya awamu ya tano inatekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi wakati wakijinadi kuomba kura mwaka 2015 na kwamba wananchi leo hii wanazungumza lugha moja ya kuiletea maendelo nchi yao. Aidha jambo linguine linalo wafurahisha wananchi wa Tanzania wakiwemo wa jimbo la Vwawa ni mapambano dhidi ya rushwa, ubadhilifu wa mali za umma, mapambano ya ufisadi na uinzi wa mali asili za Tanzania ni kigezo tosha wananchi wa jimbo la Vwawa kuendelea kuipa dhamana CCM ili kuharakisha maendeleo yao.Mwaka 2015 aliteuliwa na bunge kuwa mjumbe kwenye kamati ya hesabu za umma. Lakini pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya Wilaya kwa nafasi yake ya uwakilishi wa jimbo lake hadi sasa.

Uzoefu Kazini[hariri | hariri chanzo]

Uzoefu wa Kazi
Mwaka Wadhifa Shirika/Taasisi
2014 - 2015 Mkurugenzi wa Fedha Chuo cha usimmizi wa Fedha (IFM)
2013 - 2013 Mkuu wa Idara ya Utafiti na Ushauri Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC)
2012 - 2012 Kaimu Mtendaji Mkuu Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC)
2011 - 2013 Naibu mkuu wa Chuo fedha , Utafiti na utawala Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC)
2008 - 2011 Naibu mkuu wa Chuo Fedha na Utawala Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC)
2008 - 2014 Mhadhili mwandamizi Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC)
2003 - 2006 Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC)
2003 - 2015 Mhadhili na Mshauri Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC)
2002 - 2002 Kaimu Meneja wa Hazina Mfuko wa Taifz wa hifadhi ya Jamii (NSSF)
1998 - 2002 Mhasibu wa Kanda Mfuko wa Taifz wa hifadhi ya Jamii (NSSF)
1996 - 1998 Mhasibu wa Mkoa Mfuko wa Taifz wa hifadhi ya Jamii (NSSF)

Mafunzo[hariri | hariri chanzo]

katika maisha yake Japhet Ngailonga Hasunga meshiriki katika mafunzo mbalimbali kuhusiana na masuala ya kiutawala na menejiment,

Mafunzo Mbalimbali
Aina ya mafunzo Chuo Tovuti
Mafunzo ya Usimamizi na uongozi wa Umma Chuo cha Utawala na Uongozi https://www.ipac-edmonton.ca/awards
Mafunzo ya menejimenti na usimaamizi wa Umma Chuo cha Utawala na Uongozi https://www.ipac-edmonton.ca/awards
Mafunzo ya kubadilishana vyuo vya utumishi na Utawala Administrative Staff College of Nigeria Administrative Staff College of Nigeria (ASCON)
Mafunzo ya usimamizi wa rasilimali na mabadiliko ya tabia nchi Pennlylvania State University N/A
Mafunzo ya awali ya Shahada ya Udhamivu (PHD) Chuo cha Stellenbosch Stellenbosch University official site

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
  2. http://michuzijr.blogspot.com/2018/05/serikali-yaeleza-fursa-ya-ufugaji-wa.html
  3. https://successfulsocieties.princeton.edu/interviews/japhet-hasunga
  4. http://www.nec.go.tz/uploads/documents/sw/1513775610-21-MATOKEO%20YA%20UCHAGUZI%20MKUU%202015.pdf