Nenda kwa yaliyomo

Hedwig wa Andechs

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Hedwig akiwa na wengine, Hedwig Codex, Lubin, 1353 (sasa katika J. Paul Getty Museum, California, Marekani[1])

Hedwig wa Andechs (kwa Kijerumani: Hedwig von Andechs; pia: Hedwig wa Silesia, kwa Kipolandi: Jadwiga Śląska; Andechs, Bavaria, 1174Trzebnica Abbey, Silesia, 15 Oktoba 1243) alikuwa mwanamke wa ukoo tawala wa Andechs ambaye, kisha kuolewa na mtemi Henri Mwenyendevu, akawa malkia wa Polandi hadi mwaka 1238[2].

Alijitosa kwa bidii kuhudumia watu fukara, akijenga makazi kwa ajili yao. Kisha kubaki mjane, alitumia kwa manufaa miaka ya mwisho ya maisha yake katika monasteri ya Wasitoo ambayo alikuwa ameianzisha mwenyewe na iliongozwa na binti yake Getrude kama abesi[3].

Tarehe 26 Machi 1267 Papa Klementi IV alimtangaza mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe 16 Oktoba[4].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.