Halima James Mdee

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Halima James Mdee ni mbunge wa viti maalum katika bunge la Tanzania kupitia chama pinzani cha CHADEMA.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Halima James Mdee alizaliwa tarehe 18 Machi 1978 katika kijiji cha Makanya, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro akiwa mtoto wa mwisho katika familia ya Profesa James Mdee ambaye alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kikabila ni Mpare.

Mdee alizaliwa katika familia ya Wakristo na alibatizwa na kuitwa Theodosia, hata hivyo anatumia zaidi jina alilorithi kutoka kwa bibi yake mzaa baba, Halima.

Ukoo wake ni waumini wa dini ya Kiislamu, isipokuwa baba yake na kaka yake ambao walibatizwa na familia yao ikaridhia wawe Wakatoliki.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Alianza kusoma elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Mlimani jijini Dar es Salaam mwaka 1985 na kuhitimu mwaka 1991. Alichaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana Zanaki mwaka 1992 na kuhitimu kidato cha nne mwaka 1995.

Mwaka 1996 hadi 1998 alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kilakala mkoani Morogoro na 1999 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alisomea sheria na kuhitimu mwaka 2003.

Kazi na Siasa[hariri | hariri chanzo]

Alipata ajira katika Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana mwaka 2004 akiwa Ofisa Maendeleo kama mwanasheria mpaka mwaka 2005 alipoamua kuacha kazi na kuingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, ambako alishiriki kuwapigia kampeni wagombea mbalimbali wa CHADEMA kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa viti maalumu.

Vyeo vya Chama[hariri | hariri chanzo]

Mbali na ubunge, pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa la CHADEMA, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA na ofisa katika kurugenzi ya sheria.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]