Soya
Soya (Glycine max) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Soya
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Soya ni aina ya maharagwe na mbegu za msoya (Glycine max) katika familia Fabaceae. Asili yake iko Asia ya Mashariki.
Ni zao la mafuta na sifa yake ya pekee ni kiasi kikubwa cha protini katika mbegu zake (40-50%). Kutokana na lishe yake kubwa kilimo chake kimeenea duniani. Kwa watu wasiokula nyama, mafuta ya soya na vyakula vinavyotokana na soya yana mahitaji yote ya protini kwa gharama ndogo.
Rangi ya mbegu zake huwa ni njano, nyeupe lakini kuna pia aina za kahawia.
Utangulizi
[hariri | hariri chanzo]Mmea huu ulitumika sana huko Asia ya Mashariki kwa zaidi ya miaka 5000. Tangu karne ya 1 KK ilikuwa zao la chakula muhimu sana katika China.
Katika karne ya 18 BK soya ilipelekwa Ulaya ila haikutumiwa sana. Lakini baada ya kulimwa Marekani ilionekana kuleta mavuno mazuri katika tabianchi hiyo. Iliendelea kuwa zao lenye kiwango kikuu cha mafuta na protini na kuwa na mavuno mazuri ya mara kwa mara.
Soya huwa na kiasi kikubwa cha asidi za phtyic, alpha-Linoplenic na daidzein. Bidhaa za soya kama vile TVP (textured vegetable protein), kwa mfano, ni muhimu sana kama viungo vya mapishi mengi ya nyama na maziwa.
Mafuta ya soya hutumika kwa namna mbalimbali. Wazalishaji wakuu wa soya ni Marekani, Brazili, Ajentina, China na India.
Aina za soya
[hariri | hariri chanzo]Aina za soya hutofautiana katika ukuaji[[]], tabia na kimo. Huweza kukua chini ya sentimita 20 lakini pia huweza kukua hata zaidi ya mita 2.
Makaka ya soya, shina na majani hufunikwa na vinyweleo vya kahawia. Majani hugawanyika katika sehemu kuu tatu, huku kila jani likiwa na urefu wa sentimita 6 – 15 na upana wa sentimita 2. Majani huanguka kabla ya kukomaa kwa mbegu. Maua, yenye uwezo wa kujichavusha yenyewe, hukua katikati ya majani na huwa na rangi ya pinki, hudhurungi au nyeupe.
Tunda lake ni ganda lenye vinyweleo, ambalo hukua kwenye makundi ya maganda 3 – 5, huku kila ganda likiwa na ukubwa wa sentimita 3 – 8, na kuwa na mbegu 2 – 4 ndani yake, zenye kipenyo cha milimita 5 – 11.
Soya huja katika rangi mbalimbali, na mara nyingi katika rangi nyeusi, kahawia, bluu, njano, kijani na mchanganyiko wa rangi mbalimbali. Mbegu zilizokomaa ni ngumu, zisizopenyesha maji kwa urahisi hivyo kulinda kotiledoni na haipokotaili au kiini visiharibiwe. Kama gamba la nje la mbegu likiharibiwa, mbegu haitaota. Kovu linaloonekana kwenye mgegu hitwa hilamu, na katika mwisho mmoja wa hilamu kuna tundu dogo maalumu kwa kupitisha hewa na maji kwaajili ya kuchipua.
Kwa uthibitisho, mbegu za jamii ya mikunde, soya ikiwa miongoni mwao, huwa na aina ya protini ambayo hudumu hata baada ya kusharabu maji. A. Carl Leopold, alitafiti juu ya uwezo huu. Aligundua pia kuwa soya ina kiasi kikubwa cha kabohaidreti kinacholinda uhai wake.
Kwa pamoja, mafuta na protini vinafanya karibu 60% ya soya kavu kwa uzito; protini ikiwa 40% na mafuta 20%. Sehemu iliyobaki ni 35% kabohaidreti na 5% madini mengine mchanganyiko.
Virutubishi
[hariri | hariri chanzo]Kwa matumizi ya binadamu, soya ni chanzo cha kiaminika cha protini iliyokamilika. Na soya huwa na humeng’enywa vyema kama ikipikwa kabla ya kuliwa. Kulingana na tafiti nyingi, bidhaa za soya zimeonekana kuwa na kiwango cha protini cite kinachotakiwa tofauti na mimea mingine, soya huwa na protini inayoweza hata kuwa badala ya ile inayopatikana kwa nyama, ambayo huwa na mchanganyiko wa mafuta mengi, hivyo kuipa soya alama za juu sababu haina mafuta hayo yanayoweza kuwa hatari kwa mwili wa binadamu.
Hata hivyo, licha ya faida nyingi za kiafya bado kuna mjadala mkubwa juu ya faida za kiafya za soya katika mlo.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Majani
-
Maua
-
Ua
-
Makaka mabichi
-
Makaka mabivu
-
Soya
-
Jibini ya soya (sheese)
-
Soya zilizobanikwa
-
Mafuta ya soya
-
Unga wa soya
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- American Soybean Association
- Cornell University Food and Brand Lab
- Evaluation of Anti-Soy Data and Anti-Soy Advocates Ilihifadhiwa 5 Aprili 2007 kwenye Wayback Machine.
- Guardian - There's no risk to humans from soya
- IITA has CGIAR global mandate for Soybean research for development Ilihifadhiwa 30 Machi 2008 kwenye Wayback Machine.
- International Institute of Tropical Agriculture
- Soy information
- Soy information at Soyatech Ilihifadhiwa 15 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine.
- Soy Heart healthy claims in dispute
- Soyinfo Center - SoyaScan database and books
- Soy Protein Information
- United Soybean Board
- Concerns Regarding Soybeans Ilihifadhiwa 18 Aprili 2008 kwenye Wayback Machine.
- Guardian - Should we worry about soya in our food?
- Health Canada: Soy - One of the nine most common food allergens Ilihifadhiwa 9 Aprili 2008 kwenye Wayback Machine.
- Soy Allergy Information Page Ilihifadhiwa 22 Septemba 2015 kwenye Wayback Machine. Asthma and Allergy Foundation of America
- Soy Online Service Ilihifadhiwa 10 Aprili 2007 kwenye Wayback Machine.
Hasara za kilimo cha Soya
[hariri | hariri chanzo]- AlterNet: Health & Wellness: The Dark Side of Soy Ilihifadhiwa 16 Machi 2008 kwenye Wayback Machine.
Upishi wa soya
[hariri | hariri chanzo]- How to make soy milk (quick guidelines)
- Soya / Tofu Recipes Ilihifadhiwa 31 Machi 2008 kwenye Wayback Machine.