Glassdoor

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Glassdoor
Aina ya shirikaPrivate
Tarehe ya kwanzaJune 2007
MwanzilishiRobert Hohman, Rich Barton, Tim Besse
Pahali pa makao makuuMill Valley, California, U.S.
Sekta ya viwandaInternet
HudumaOnline employment
Wafanyakazi800
Tovutiglassdoor.com
Daraja la AlexaKigezo:DecreasePositive 397 (October 2017)[1]
Aina ya tovutiJob search engine, Review Site
KusajiliOptional
LughaMultilingual
Hali ya sasaActive
Tovuti ya Glassdoor

Glassdoor ni tovuti ambayo wafanyakazi au waliokuwa wafanyakazi wa kampuni wanatoa kwa siri maoni yao kuhusu kampuni hiyo.[2]

Mnamo Mei 2018, Recruit Holdings, kampuni ya Kijapani ambayo pia inamiliki tovuti ya matangazo ya kazi ya Indeed ilitangaza nia yake ya kuinunua kampuni ya Glassdoor kwa dola za Kimarekani bilioni 1.2.[3]

Kuanzishwa[hariri | hariri chanzo]

Glassdoor ilianzishwa mwaka 2007 na Tim Besse, Robert Hohman, ambaye ndiye Mkurugenzi wa kampuni, na Rich Barton, mwanzilishi wa kampuni ya Expedia.

Tovuti[hariri | hariri chanzo]

Tovuti ya Glassdoor ilizinduliwa rasmi Juni 2008,[4] kama tovuti inayokusanya maoni kwa siri kuhusu kampuni na mishahara ya wafanyakazi. Kati ya kampuni kubwa zilizotokea kwenye tovuti hiyo ni Google na Yahoo.[5] The site also allows the posting of office photographs and other company-relevant media.[6]

Hadi mwaka 2015, tovuti hiyo ilikuwa na watumiaji milioni 30 toka nchi 190.[6] Mwaka huo, kampuni hii ilianza kufungua tovuti na apps zinazolenga mataifa mbalimbali kama vile Ujerumani.[7]

Mnamo Septemba 2016, Glassdoor ilinunua kampuni ya Brazili ya Love Mondays ili kujiimarisha katika nchi za Amerika ya Kusini.[8]

Takwimu za tovuti hiyo mwanzoni mwa mwaka 2017 zinaonyesha ilikuwa na watumiaji milioni 41 na wateja 5,800.

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Aprili 2013, Glassdoor ilishinda tuzo ya Red Herring.[9]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Glassdoor kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.