Funguvisiwa la Malay

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Funguvisiwa ya Malay)
Funguvisiwa la Malay.
Mahali pake.

Funguvisiwa la Malay (kwa lugha kubwa za wenyeji: Nusantara, Kapuluang Malay, Kapupud-ang Malay) ni funguvisiwa lililoko kati ya Indochina na Australia[1].

Jumla ya visiwa ni zaidi ya 25,000. Nchi zifuatazo zina maeneo katika funguvisiwa hili:

Watu zaidi ya milioni 380 wanaishi juu yake. [2]

Kisiwa chenye watu wengi ni Java kikiwa na watu milioni 141. Kisiwa kikubwa ni Borneo (Kalimantan) ambako zinakutana nchi tatu za Indonesia, Malaysia na Brunei. Vingine vikubwa ni Sumatra, Sulawesi na Java huko Indonesia; pamoja na Luzon na Mindanao huko Ufilipino.

Kisiwa kikubwa cha New Guinea kwa kawaida hakihesabiki ndani ya funguvisiwa la Malay.

Funguvisiwa hilo ni kati ya sehemu za dunia zenye volkeno hai zaidi duniani.

Tabianchi ni ya kitropiki kutokana na ikweta kupita katikati ya eneo hilo.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Wallace, Alfred Russel (1869). The Malay Archipelago. London: Macmillan and Co. p. 1. 
  2. Encyclopædia Britannica. 2006. Chicago: Encyclopædia Britannica, Inc.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Funguvisiwa la Malay kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Coordinates: 2°56′S 107°55′E / 2.933°S 107.917°E / -2.933; 107.917