Funguvisiwa la Lamu

Majiranukta: 2°06′12″S 41°01′14″E / 2.10333°S 41.02056°E / -2.10333; 41.02056
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya funguvisiwa la Lamu: Lamu, Manda, Pate.

Funguvisiwa la Lamu ni kundi la visiwa katika Bahari Hindi mbele ya pwani ya Kenya kaskazini ambavyo ni sehemu ya Kaunti ya Lamu, Kenya.

Visiwa vikubwa ni Pate, Manda na Lamu. Visiwa vidogo ni pamoja na Kiwayu na Manda Toto.

Mji mkubwa zaidi ni Lamu kwenye Kisiwa cha Lamu. Mji huu uko katika orodha ya Urithi wa dunia ya UNESCO.

Funguvisiwa la Lamu lina sehemu mbalimbali zenye mabaki muhimu ya kiakiolojia kutoka vyanzo vya utamaduni wa Waswahili kama vile Takwa na mji wa Manda halafu Shanga, Pate.

Kuna taarifa ya kwamba jahazi za kundi la meli la Zheng He zilizama karibu na Lamu mnamo mwaka 1415.[1] Mabaharia wa jahazi hizi walibaki kwenye visiwa na kuoa wanawake wa huko. Uchunguzi wa DNA wa wenyeji umethibitisha kuwepo kwa damu ya Kichina.[2] [3][4]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Engel, Ulf; Ramos, Manuel João (17 May 2013). African Dynamics in a Multipolar World. BRILL. ISBN 978-90-04-25650-7.
  2. Eliot, uk. 11
  3. "Kenyan girl with Chinese blood steals limelight". Chinese Embassy in Kenya. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo May 8, 2013. Iliwekwa mnamo 3 April 2009.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  4. Kristof, Nicholas D.. "1492: The Prequel", The New York Times, 6 June 1999. Retrieved on 3 April 2009. 

Kujisomea[hariri | hariri chanzo]

  • Allen, James de Vere: Lamu, with an appendix on Archaeological finds from the region of Lamu by H. Neville Chittick. Nairobi: Kenya National Museums.
  • Eliot, Charles (1966). The East African Protectorate. Routledge. ISBN 0-7146-1661-3. 
  • Engel, Ulf; Ramos, Manuel João (17 May 2013). African Dynamics in a Multipolar World. BRILL. ISBN 978-90-04-25650-7.  Check date values in: |date= (help)
  • Martin, Chryssee MacCasler Perry; Martin, Esmond Bradley: "Quest for the Past: An Historical Guide to the Lamu Archipelago" Marketing and Publishing Ltd., 1973.

2°06′12″S 41°01′14″E / 2.10333°S 41.02056°E / -2.10333; 41.02056