Nenda kwa yaliyomo

Lamu (kisiwa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Funguvisiwa la Lamu: Lamu, Manda, Pate.
Mahali pa Lamu katika Kenya.

Kisiwa cha Lamu ni sehemu ya funguvisiwa la Lamu pamoja na visiwa vya Pate na Manda karibu na mwambao wa Kenya katika Bahari Hindi.

Kisiwani Lamu kuna mji wa Lamu na vijiji vya Shela, Kipangani na Matondoni. Shela imekuwa mahali pa utalii ambako watu wa nje wamejenga nyumba zao. Matondoni bado ni kijiji cha Waswahili watupu wanaojenga jahazi kama zamani.

Lamu inafikiwa kwa njia ya barabara ya pwani kutoka Malindi halafu kwa feri ya Mukowe. Kuna mabasi kadhaa kila siku tangu kuboreshwa kwa barabara kulipopunguza matatizo ya ujambazi njiani. Watalii wengi wanafika kwa njia ya ndege. Uwanja wa ndege wa kitaifa upo Manda kisiwani na abiria huvuka kwa maboti.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kuhusu historia ya Lamu tazama makala ya mji wa Lamu.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]