Nenda kwa yaliyomo

Frances Ames

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Frances Rix Ames ( /ˈfrɑːnsɪz//mz/; 20 Aprili 192011 Novemba 2002) alikuwa bingwa wa nyuroni, daktari wa magonjwa ya akili, na mpiganaji wa haki za binadamu nchini Afrika Kusini.

Amefahamika kwa ubora wake katika kuongoza uchunguzi wa kifo cha mwanaharakati Steve Biko aliyepinga ubaguzi wa rangi, ambaye alikufa kutokana na matibabu kutelekezwa na kuteswa chini ya ulinzi wa polisi. Pindi ambapo baraza la matibabu la Afrika ya Kusini (SAMDC) liliposhindwa kuwachukulia hatua za kinidhamu daktari mkuu wa upasuaji wa wilaya na msaidizi wake ambao walihusika na matibabu ya Steve Biko, Ames na wenzake watano (wasomi na madaktari) walichangisha fedha na kupambana vita halali kisheria ya takribani miaka minane kupinga kuanzishwa kwa matibabu. Ames alihatarisha usalama wa maisha yake na kazi yake, kwa ajili ya kupigania haki, na kuipeleka kesi mahakama kuu ya Afrika ya kusini (South African Supreme Court) ambapo hatimaye alishinda kesi hiyo mwaka 1985.

Alizaliwa Pretoria na kukulia katika umaskini katika mji wa Cape Town. Ames alikuwa mwanamke wa kwanza kupokea shahada ya Udaktari wa Dawa kutoka chuo Kikuu cha Cape Town mwaka 1964.

Ames alisoma madhara ya bangi kwenye ubongo na kuchapisha makala kadhaa juu ya somo hilo; kuona faida ya matibabu ya bangi juu ya wagonjwa katika hospitali yake mwenyewe. Aliwahi kuwa mtetezi wa kuhalalisha kwa matumizi ya dawa.

Aliongoza idara ya neurolojia ya Hospital ya Groote Schuur kabla ya kustaafu mwaka 1985, lakini aliendelea kufundisha katika Hospitali za Valkenberg na Alexandra.

Baada ya ubaguzi wa rangi kumalizika mwaka 1994, Ames alitoa ushahidi mbele ya tume ya Ukweli na Maridhiano juu ya uchunguzi wa "Madaktari wa Biko" kwa kukiuka maadili ya matibabu.

Mwaka 1999, Nelson Mandela alimzawadia Ames tuzo ya Nyota wa Afrika Kusini, ambayo ni tuzo ya juu kabisa kwa raia wa Afrika ya kusini.