Fatima Massaquoi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Fatima Massaquoi mnamo 1928.

Fatima Massaquoi-Fahnbulleh (19121978) alikuwa kati ya waanzilishi wa elimu ya juu nchini Liberia.

Akizaliwa katika ukoo wa wafalme wa kikabila akiwa mtoto wa balozi wa kwanza Mwafrika katika Ujerumani akapata elimu yake huko Ujerumani, Uswisi na Marekani.

Baada ya kurudi Liberia alikuwa kati ya walimu waliojenga chuo kikuu cha kwanza cha Liberia na kuchangia mengi katika utamaduni wa nchi.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Utoto katika Liberia[hariri | hariri chanzo]

Alikozaliwa alikuwa mtoto wa nane wa Mamalu Massaquoi, mwene wa Wavai, kabila la pande zote mbili za mpaka kati ya Sierra Leone na Liberia.

Alilelewa na shangazi kwa miaka ya kwanza akaanza kusoma shule Liberia.

Kijana katika Ujerumani na Uswisi[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1922 alipokuwa na umri wa miaka 10 hivi baba yake alitumwa kwenda Hamburg, Ujerumani akiwa konsuli mkuu na hivyo balozi wa kwanza Mwafrika katika Ulaya bara. Alimteua binti yake Fatima aje naye.

Fatima alikaa Ujerumani hadi mwaka 1937. Huko alijifunza haraka Kijerumani alisoma kwenye shule za St Ansgar na Helene Lange mjini Hamburg hadi kufikia mtihani wa Abitur ya Kijerumani inayolingana na Form VI. Alikaa pia kwa miaka kadhaa Uswisi alipojifunza Kifaransa.

Mwaka 1933 siasa ya Ujerumani ilibadilika, na chama cha Nazi chini ya Adolf Hitler kilianzisha udikteta wake. Ubaguzi wa kimbari ulienea, hasa dhidi ya Wayahudi, lakini hali kwa Waafrika ilianza kuwa vigumu pia.

Masomo katika Marekani[hariri | hariri chanzo]

Hapo Fatima aliamua kuhamia Marekani aliposoma Lane College, Fisk University na Chuo Kikuu cha Boston. Alisoma elimu ya jamii na kupata digrii ya bachelor na digrii mbili za uzamili. Alishiriki pia katika kutunga kamusi ya Kivai, lugha mama yake.

Kurudi Liberia[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1946 alirudi Liberia akaanza kushiriki katika juhudi za kuanzisha chuo kikuu cha kwanza cha nchi hiyo.

Alikuwa mkurugenzi na baadaye mkuu wa Liberal Arts College. Aliunda Taasisi ya Utafiti wa Kiafrika. Alishiriki kuanzisha shirika la waandishi wa Liberia. Alipigania fesheni ya kubadilisha majina ya Kiafrika kwa majina ya Kizungu wakati wa kujiandikisha chuoni. Alipinga ubaguzi uliokuwepo dhidi ya Waliberia kutoka jamii za kikabila kwa upande wa waanzilishi wa Liberia ambao mababu wao walikuwa Wamarekani weusi.

Mwaka 1978 aliaga dunia kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu.

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fatima Massaquoi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.