Nenda kwa yaliyomo

F. Gary Gray

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
F. Gary Gray
Gray at ComicCon, 2015
Amezaliwa17 Julai 1969 (1969-07-17) (umri 55)
Kazi yakeMwongozaji wa filamu, mtayarishaji wa filamu, mwongozaji wa muziki wa video, mwigizaji
Miaka ya kazi1989–hadi sasa

Felix Gary Gray (amezaliwa 17 Julai, 1969) ni mwongozaji wa filamu, mtayarishaji wa filamu, mwongozaji wa video za muziki na mwigizaji kutoka nchini Marekani.[1] Gray ameongoza Friday, Set It Off, The Negotiator, The Italian Job, Straight Outta Compton, vilevile The Fate of the Furious ya mwaka wa 2017.[2]

Maisha na kazi

[hariri | hariri chanzo]

Gray ni mzaliwa wa mjini New York. Alianza kazi yake mnamo mwaka wa 1989 aliponekana katika filamu ya vichekesho Major League. Miaka mitatu baadaye, akaongoza video ya muziki ya Ice Cube "It Was a Good Day". Video ni gezeo la mashairi yake. Hatimaye baadaye akawa muongozaji mzuri tu wa video zingine kutoka kwa Ice Cube, vilevile wasanii wengine kama vile Cypress Hill, Outkast, Dr. Dre, na Queen Latifah.

Akiwa na umri wa miaka 24, Gray akaongoza filamu filamu yake ya kwanza, vichekesho vya mjini Friday akiwa na rapa-mwigizaji Ice Cube na Chris Tucker. Baadaye akaja kuongoza filamu ya Set It Off, akiwa na Jada Pinkett na Queen Latifah. Kisha akaongoza The Negotiator, ambayo imechezwa na mshindi wa tuzo za Acadamy Kevin Spacey na mmoja wa waliowahi kushindanishwa katika tuzo za Academy Award-Samuel L. Jackson, na hapo ndipo alipopata tuzo-2 ya mwongozaji na filamu bora 1998 katika Tamasha la Filamu la Acapulco.

Gray pia aliongoza filamu ya The Italian Job, filamu ya kusisimu iliyochezwa na mshindi wa Tuzo za Academy Charlize Theron na mtajwa kwenye tuzo hizo Mark Wahlberg. Gray alipata kusifika kama mwongozaji bora wa filamu hiyo mwaka wa 2004 katika Tamasha la Filamu la Wamarekani Weusi, ambayo ilivuka dola milioni $100 katika box office ya nchini humo.

Filamu yake iliyofuata ilikuwa A Man Apart, a filamu ya kusisimua na fujo ndani yake ilichezwa na Vin Diesel. Baadaye akaongoza Be Cool, gezo lingine la riwaya ya Elmore Leonard yenye jina hilohilo Be Cool. Sifa kubwa alipata John Travolta, lakini filamu imeingiza kiasi cha dola za Kimarekani milioni 95.2 dunia nzima.

Filamu engine iliyofuata ilikuwa Law Abiding Citizen, iliyochezwa na nyota mshindi wa Tuzo za Academy Jamie Foxx na Gerard Butler. Muswaada andishi uliandikwa na Kurt Wimmer, na imeingiza dola za Kimarekani milioni 100 kwa hesabu ya dunia nzima.

Gray pia anahusika kwa kuongoza video za muziki mbalimbali. Alipata kufanya kazi na TLC, Dr. Dre, Tupac Shakur, Mary J. Blige, Stevie Wonder, Babyface, na Jay-Z, na wengine wengi.

Gray alipata tuzo ya The Ivan Dixon Award of Achievement kutoka kwa Black Hollywood Education and Resource Center na kutajwa kama “50 Best and Brightest African Americans Under 40” (yaani, Vijana Bora 50 wa Wamarekani Weusi Waliochini ya Miaka 40) na jarida la Black Enterprise. Vilevile alitunukiwa tuzo ya heshima na African American Film Critics Association kwa toleo lao mahususi la mwaka wa 2004 lililoitwa Special Achievement Award na alitambuliwa na "Artist Empowerment Coalition with the Artist Empowerment Award" katika mwaka huohuo. Vilevile alipata tuzo ya Pioneer Director kutoka kwa Pan-African Film and Arts Festival mnamo 2010.

Vilevile ameongoza igizo bab-kubwa la Straight Outta Compton, ambayo ilikuwa filamu ya wasifu wa kundi la rap maarufu kama N.W.A.

Gray alichaguliwa kama mwongozaji wa filamu ya The Fate of the Furious ambayo itatoka tarehe 14 Aprili, 2017.[3]

Filmografia

[hariri | hariri chanzo]

Filamu alizoshiriki

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Filamu Mwongozaji Mtayarishaji Mengineyo Maelezo
1995 Friday Ndiyo Hapana Ndiyo Cameo as “Black Man at Store”
1996 Set It Off Ndiyo Ndiyo Ndiyo Gangster talking to Cleo in the lowrider
1998 The Negotiator Ndiyo Hapana Hapana
1999 Ryan Caulfield: Year One Ndiyo Ndiyo Hapana Television pilot
2003 The Italian Job Ndiyo Hapana Hapana
A Man Apart Ndiyo Ndiyo Hapana
2005 Be Cool Ndiyo Ndiyo Hapana
2009 Law Abiding Citizen Ndiyo Hapana Hapana
2015 The Sea of Trees Hapana Ndiyo Hapana
Straight Outta Compton Ndiyo Ndiyo Ndiyo Cameo as “Greg Mack”
2017 The Fate of the Furious Ndiyo Hapana Hapana
2019 Men in Black: International[4] Ndiyo Hapana

Anaoshirikiana nao mara kwa mara

[hariri | hariri chanzo]
Mwigizaji Friday (1995) Set It Off (1996) The Negotiator (1998) A Man Apart (2003) The Italian Job (2003) Be Cool (2005) Straight Outta Compton (2015) The Fate of the Furious (2017) Jumla
Ice Cube NoN NoNProducer 2
Vin Diesel NoN NoN 2
Paul Giamatti NoN NoN 2
Seth Green NoN NoN 2
Anna Maria Horsford NoN NoN 2
Dwayne Johnson NoN NoN 2
Jason Statham NoN NoN 2
Charlize Theron NoN NoN 2

Video za muziki

[hariri | hariri chanzo]
  1. "F Gary Gray", The New York Times. Retrieved on August 19, 2015. 
  2. "Fast & Furious 8 (2017) - IMDbPro".
  3. "The Fate of the Furious (2017) - Box Office Mojo".
  4. Chitwood, Adam (2018-12-05). "The 'Men in Black' Reboot Is Titled 'Men in Black International'". Collider (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2018-12-05.
  5. ""Pretty Girl" by Jon B. | Music Video | VH1.com". VH1. Viacom International. Septemba 1, 2004. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-05-18. Iliwekwa mnamo Mei 9, 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]