Nenda kwa yaliyomo

Natural Born Killaz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Natural Born Killaz”
“Natural Born Killaz” cover
Single ya Dr. Dre na Ice Cube
kutoka katika albamu ya Murder Was the Case
Imetolewa 1994US1995EU
Muundo 12" singleUS, CD5EU
Aina Gangsta rap, G Funk, Horrorcore
Urefu 4:15
Studio Death Row/Interscope
Mtayarishaji Dr. Dre, Sam Sneed, Suge Knight (exec.)
Certification Gold (RIAA)
Mwenendo wa single za Dr. Dre
"Who Am I (What's My Name)?"
(1993)
"Natural Born Killaz"
(1994)
"Keep Their Heads Ringin'"
(1995)
Mwenendo wa single za Ice Cube
"You Know How We Do It"
(1994)
"Natural Born Killaz"
(1994)
"Bop Gun (One Nation)"
(1994)

"Natural Born Killaz" ni single kutoka kwa muungano wa wasanii wawili ambao ni Dr. Dre na Ice Cube. Awali ilinuiwa kwa ajili ya albamu iliyotiwa kapuni ya 'Heltah Skeltah'. Hii ndio mara ya kwanza kwa wawili hawa kuwa pamoja katika single moja tangu enzi za kundi lao la rap N.W.A lilipogawanyika.

Single ilitolewa mnamo mwaka wa 1994 huko nchini Marekani na mwaka wa 1995 huko nchini Uingereza. Kwenye upande wa matayarisho kunashirikishwa Soopafly katika upande wa vinanda na Jewell kwenye upande sauti. Kitangulizi (makadirio yake sekunde 30 kuzidi urefu halisi) wanaoneshwa mume na mke wakielekea nyumbani kupitia kichochoro kisichokaliwa na watu, ambapo walikuwa wakifuatwa kwa nyuma wakaanza kulumbana na na wakazi wa pale.

Japokuwa kitangulizi ni tofauti kwenye video na toleo la sauti yote mawili yanahusisha mauaji na mwishowe kuna sikika sauti ya bunduki. Japokuwa wimbo na video zilitolewa na zimepata umaarufu mkubwa tu sawa na kutolewa kwa filamu ya Oliver Stone, Natural Born Killers, lakini wimbo haujaonekana kwenye filamu hiyo.

Toleo la EP la UK[hariri | hariri chanzo]

  1. Ice Cube and Dr. Dre - Natural Born Killaz (Radio Edit) (4:16)
  2. Ice Cube and Dr. Dre - Natural Born Killaz (Video Edit) (6:33)
  3. Ice Cube and Dr. Dre - Natural Born Killaz (LP Version) (4:52)
  4. Tha Dogg Pound - What Would You Do? (LP Version) (5:09)

Toleo la EP la Marekani[hariri | hariri chanzo]

  1. Dr. Dre & Ice Cube - Natural Born Killaz (Radio Version) (4:15)
  2. Dr. Dre & Ice Cube - Natural Born Killaz (LP Version) (4:50)
  3. Sam Sneed feat. Dr. Dre - U Better Recognize (LP Version) (3:55); #16 Billboard Hot Dance Music/Maxi-Singles Sales chart, #18 Hot Rap Singles chart.

Albamu zenye wimbo huu[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]