Keep Their Heads Ringin'

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Keep Their Heads Ringin'”
“Keep Their Heads Ringin'” cover
Single ya Dr. Dre
kutoka katika albamu ya Friday
B-side "Take a Hit" by Mack 10
Imetolewa 7 Machi 1995
Muundo CD single, CD maxi, 12" single
Imerekodiwa 1995
Aina West Coast Rap
Urefu 5:06
Studio Priority
Mtunzi Angie Stone, G. Chisholm, C. Cooks,
A. Young, James E. Anderson, S. Robinson,
S. Anderson
Mtayarishaji Dr. Dre na Sam Sneed
Mwenendo wa single za Dr. Dre
"Natural Born Killaz"
(1995)
"Keep Their Heads Ringin"
(1995)
"California Love"
(1996)

"Keep Their Heads Ringin'" (wakati mwingine hutajwa kimakosa kama Ring Ding Dong) ni jina la kutaja single ya Dr. Dre iliyochukuliwa kutoka katika kibwagizo cha filamu ya Friday.[1] Ijapokuwa albamu ilitolewa kupitia Priority Records, Death Row Records bado wanamiliki nakala kuu ya wimbo huu. Wimbo uliingia nafasi ya 10 kwenye chati za Billboard Hot 100 na ulitunukiwa dhahabu na RIAA mnamo tar. 10 Mei 1995 kwa mauzo zaidi ya 500,000.

Pia imefikia nafasi ya kwanza kwenye chati za Hot Rap Tracks huko nchini Marekani. Wimbo umetia maneno ya "Funk You Up" wa The Sequence kutoka katika single yao ya mwaka wa 1980 iliyotolewa chini ya Sugar Hill. Wimbo pia umeonekana kwenye Death Row Greatest Hits iliyotolewa mnamo mwaka wa 1996. Kitangulizi cha "Hey. Whatup?" kimefanywa na Dr. Dre wakati kiendelezo cha kifunguzi chenye muziki kuna KRS-One anasema nembo ya biashara yake kwa zogo "Buck, buck, buck".

Matoleo tofauti[hariri | hariri chanzo]

Kuna toleo lingine la wimbo ambalo linaweza kupatikana kwenye Death Row Greatest Hits na albamu ya kompilesheni ya Death Row Dayz, ambapo Dr. Dre ametumia mistari hii:

Just chill, listen to the beats I spill
I use Crest, so ain't no cavity creeps in my grill

Badala ya toleo ambalo linatumika zaidi la:

Just chill, listen to the beats I spill
Keepin' it real, enables me to make another mill' [mill' is short for million]

Muziki wa video[hariri | hariri chanzo]

Muziki w video ulitayarishwa na F. Gary Gray na umechukua nafasi kwenye banda la ndege, ndani ya Convair 880, kukiwa na Dr. Dre, na kundi lake likishika-hatamu usimamizi na udhibiti wa mwendendo wa ndege. Video inashikisha wanachama kadhaa wa kwenye filamu ya Friday ikiwa ni pamoja na Chris Tucker, Faizon Love, na Nia Long. Video inaishia na Chris Tucker na Faizon Love wanachukua ndege na kupaa nayo wakikimbia mapolisi. Chris Tucker anasema "I'm on probation, I can't go back to jail" anakumbukuia uhusika wa Smokey ambaye alikuwa na matata ya kisheria kwenye Friday.

Orodha ya nyimbo[hariri | hariri chanzo]

CD maxi / 12" maxi
  1. "Keep Their Heads Ringin'" (LP version) — 5:01
  2. "Keep Their Heads Ringin'" (instrumental) — 4:57
  3. "Take a Hit" (by Mack 10) (LP version) — 4:34
  4. "Take a Hit" (by Mack 10) (instrumental) — 4:34
CD single
  1. "Keep Their Heads Ringin'" (LP version) — 5:01
  2. "Take a Hit" (by Mack 10) (LP version) — 4:34

Chati[hariri | hariri chanzo]

Nafasi iliyoshika[hariri | hariri chanzo]

Chart (1995) Nafasi
iliyoshika
Belgian (Wallonia) Singles Chart[2] 15
Dutch Top 40[3] 11
Eurochart Hot 100 37
French SNEP Singles Chart[2] 29
German Singles Chart[4] 23
New Zealand RIANZ Singles Chart[2] 3
Swedish Singles Chart[2] 7
Swiss Singles Chart[2] 7
UK Singles Chart[5] 25
U.S. Billboard Hot 100[6] 10
U.S. Billboard Hot Dance Club Play[6] 4
U.S. Billboard Hot R&B/Hip-Hop Singles & Tracks[6] 10
U.S. Billboard Rhythmic Top 40[6] 13

Chati za mwishoni mwa mwaka[hariri | hariri chanzo]

Chati za mwishoni mwa mwaka (1995) Nafasi
Dutch Top 40[3] 83
French Singles Chart[7] 72
U.S. Billboard Hot 100[8] 53

Thibitisho[hariri | hariri chanzo]

Nchi Thibitisho Tarehe Tunukio za mauzo
U.S.[9] Gold 10 Mei 1995 500,000

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. King, Alex P. (2004). Hit-parade — 20 ans de tubes (in French). Paris: Pascal. p. 338. ISBN 2-35019-009-9. 
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 "Keep Their Heads Ringin'", in various singles charts Lescharts.com (Retrieved 12 Januari 2009)
  3. 3.0 3.1 Single top 100 over 1995 (pdf) (Dutch). Top40. Iliwekwa mnamo 17 Aprili 2010.
  4. Dr.Dre singles, German Singles Chart (German). musicline. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-05-08. Iliwekwa mnamo 17 Aprili 2010.
  5. UK Singles Chart Chartstats.com (Retrieved 12 Januari 2009)
  6. 6.0 6.1 6.2 6.3 Billboard Allmusic.com (Retrieved 12 Januari 2009)
  7. 1995 French Singles Chart Disqueenfrance.com Archived 7 Machi 2012 at the Wayback Machine. (Retrieved 30 Januari 2009)
  8. Billboard Top 100 - 1995. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-08-15. Iliwekwa mnamo 2010-08-27.
  9. U.S. certifications riaa.com (Retrieved 12 Januari 2009)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]