Nenda kwa yaliyomo

Aftermath Entertainment

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Aftermath Entertainment
Shina la studio Universal Music Group
Imeanzishwa 1996
Mwanzilishi Dr. Dre
Usambazaji wa studio Interscope Geffen A&M
(Nchini Marekani)
Polydor Records
(Nchini Uingereza)
Universal Music Group
(Dunia Nzima)
Aina za muziki Hip hop
Nchi Marekani
Mahala Santa Monica, California
Tovuti aftermathmusic.com

Aftermath Entertainment ni studio ya kurekodi iliyoanzishwa na msanii na mtayarishaji wa muziki wa hip hop Dr. Dre. Inafanya kazi kama kampuni tanzu na vilevile kusambaziwa kazi zake kupitia kampuni ya Interscope Records ambayo ni mali ya Universal Music Group.

Washirika waliopo sasa ni pamoja na Dr. Dre mwenyewe, Eminem, Kendrick Lamar na Jon Connor ikiwa na wasanii wa zamani akiwemo 50 Cent, Busta Rhymes, Game, Eve, Raekwon, Rakim, Slim the Mobster, Stat Quo na wengine wengi tu. Studio imefanya kazi miaka kadhaa na kujipatia tunukio kadha wa kadha za platinum 16 au zaidi katika matoleo yake yote ya albamu 20.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Alipoondoka Death Row Records mnamo Machi 22, 1996, Dr. Dre alianzisha Aftermath Entertainment kupitia Interscope Records.[1] Albamu ya Dr. Dre Presents: The Aftermath ilitolewa mwishoni mwa mwaka wa 1996 ikishirikisha wasanii ambao walikuwa miongoni mwa washirika wa mwanzo wa lebo hiyo. Mnamo mwaka wa 1997, Aftermath ilitoa albamu pekee ya kushirikiana ya kundi la muziki wa hip hop la The Firm (liliundwa na Nas, Foxy Brown, AZ na Nature). Licha ya albamu kuhusisha utayarishaji kutoka kwa Dr. Dre mwenyewe na kushika nafasi ya juu kwenye chati ya Billboard 200 na kuthibitishwa kuwa platinamu, ilikuwa na mauzo chini ya matarajio ya kibiashara na baadae kundi lilisambaratika.

Baada ya mapendekezo kutoka kwa mkurugenzi wa Interscope Jimmy Iovine, Dr. Dre alimsaini Eminem mnamo Machi 9, 1998.[2] Mwaka uliofuata (1999), albamu ya kwanza ya Eminem, The Slim Shady LP ilitolewa. Albamu ilishika nafasi ya pili kwenye Billboard 200 na nambari moja kwenye chati ya "Top R&B/Hip-Hop Albums". Albamu hii imethibitishwa kuwa platinamu mara nne, na bila shaka ndio albamu ya kwanza yenye mafanikio katika lebo hiyo. Mwaka 1999, Aftermath ilitoa 2001, ni albamu ya pili ya Dr. Dre baada ya "The Chronic". Albamu hii imethibishwa kifikisha mauzo ya platinamu mara sita.

Wasanii wengine kadhaa walisainiwa na baadaye wakaondoka kwenye lebo ya Aftermath, baadhi ya wasanii hao ni pamoja na Hittman na Rakim kutokana na migogoro ya utayarishaji. Matatizo ya kisheria yalimlazimu mwimbaji Truth Hurts kuondolewa katika lebo baada ya kutolewa kwa albamu yake.[3]

Mnamo 2002, rapa kutoka jiji la New York 50 Cent alisainiwa na Aftermath na Dr. Dre baada ya kusainiwa na Interscope kupitia Shady Records ya Eminem.[4] Albamu ya kwanza ya 50 Cent ya Get Rich or Die Tryin' ilitolewa mnamo Februari 6, 2003 kupitia Aftermath. Albamu ya Get Rich Or Die Tryin' ilihusisha utayarishaji wa Dr. Dre, ambaye pia alikuwa mtayarishaji mkuu wa albamu hiyo. Kutokana na mafanikio ya wimbo wa 21 Questions, albamu ilishika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya Billboard Top 200. Kwa kuuza nakala 872,000 katika wiki yake ya kwanza, albamu hiyo iliidhinishwa kufikisha mauzo ya platinamu mara 9 nchini Marekani mwaka wa 2020.

Game, ambaye alisainiwa na lebo hiyo mwaka 2003, alitoa albamu yake ya kwanza ya The Documentary kwa ubia na G-Unit Records mwaka 2005. Muda mfupi baada ya kutoka kwa albamu ya "The Documentary", ulizuka mvutano kati ya The Game na 50 Cent na kusababisha The Game kuondoka kwenye lebo mwaka wa 2006.

Busta Rhymes pia alitiwa saini na lebo hii na kuachia albamu moja kabla ya baadaye kuondoka kwenye lebo kutokana na mzozo na mkurungezi wa Interscope, Iovine. Albamu yake ya Back on My B.S. ilipangwa kutolewa na Aftermath. Baadae aliposaini mkataba na Universal Motown iliripotiwa kwamba albamu hiyo itatolewa kwenye lebo yake, Flipmode Entertainment, kupitia mkataba wake na Universal Motown.[5] Stat Quo pia aliondoka kwenye lebo hii mwaka wa 2008, chanzo kikitajwa kuwa ni tofauti za mwelekeo wa kisanaa.[6]

Mnamo Januari 2010, ilitangazwa kwamba Bishop Lamont ameachana na lebo hiyo kutokana na kuchelewa mara kwa mara kwa albamu yake ya kwanza, The Reformation,[7] wakati huo huo mwimbaji wa muda mrefu wa Aftermath, Marsha Ambrosius, pia alikuwa ameachana na lebo hiyo.[8]

Mnamo Machi 8, 2012, ilitangazwa kuwa Kendrick Lamar alikuwa amesaini rasmi na lebo hiyo.[9]

Mnamo Oktoba 15, 2013, Jon Connor alitangaza kusaini kwake na Aftermath wakati wa Tuzo za BET Hip Hop za 2013.[10]

Mnamo Februari 20, 2014, 50 Cent alitangaza kuachana na mkataba wake na Interscope ambao ulijumuisha mkataba wake na Aftermath na Shady.[11]

Tarehe 7 Agosti 2015, Dr. Dre alitoa albamu yake, Compton. [12]

Wasanii wa sasa

[hariri | hariri chanzo]
Msanii Mwaka
aliosainiwa
Matoleo

chini ya lebo

Dr. Dre Mwanzilishi 2
Eminem 1998 11
Kendrick Lamar 2012 5
Anderson .Paak[13] 2016 2
Silk Sonic 2021 1

Wasanii wa zamani

[hariri | hariri chanzo]
Msanii Miaka ndani
ya lebo
Matoleo
chini ya lebo
Group Therapy 1996—1997
The Firm 1996—1998 1
RBX 1996—1999
King T 1996—2001
Dawn Robinson 1997—2001
Hittman 1998—2000
Rakim[14] 2000—2002
The Last Emperor 2000—2003
Truth Hurts 2001—2003 1
50 Cent[15] 2002—2014 5
The Game 2003—2006 1
Stat Quo 2003—2008
Eve 1998
2004—2007
Busta Rhymes 2004—2008 1
Dion[16] 2005—2007
G.A.G.E.[17] 2005—2007
Raekwon 2005—2008
Bishop Lamont 2005—2010
Joell Ortiz 2006—2008
Marsha Ambrosius 2006—2009
Hayes[18] 2009—2010
Slim the Mobster 2009—2012
Jon Connor 2013—2019
Justus 2015—2016

Watayarishaji muziki wa sasa

[hariri | hariri chanzo]

Watayarishaji muziki wa zamani

[hariri | hariri chanzo]
 1. "A&R, Record Label / Company, Music Publishing, Artist Manager and Music Industry Directory". web.archive.org. 2019-01-03. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-01-03. Iliwekwa mnamo 2022-08-02.
 2. XXL StaffXXL Staff. "The #8 Biggest Moment: Eminem Signs To Aftermath - XXL". XXL Mag (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-08-02.
 3. "Truth Hurts | Aftermathmusic.com". web.archive.org. 2012-05-29. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-29. Iliwekwa mnamo 2022-08-02.
 4. "50 Cent Parts Ways with Interscope Records, Signs Independent Deal with Caroline/Capitol/UMG". Complex (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-08-02.
 5. defsounds (2008-09-15). "Busta Rhymes Inks New Deal, Jay Z Starts Yet Another Label?". Defsounds (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-08-16. Iliwekwa mnamo 2022-08-02.
 6. https://hiphopdx.com, HipHopDX -, "Stat Quo To Release "300-400" Unreleased Dr. Dre Tracks", HipHopDX (kwa American English), iliwekwa mnamo 2022-08-02 {{citation}}: External link in |last= (help)
 7. "Aftermath Music dot com | Dr. Dre Eminem 50 Cent Busta Rhymes Stat Quo Eve Bishop Lamont G.A.G.E." www.tenerifehotel.net. Iliwekwa mnamo 2022-08-02.
 8. "In Her Own Words: Marsha Ambrosius on signing to J Records + New Album | SoulCulture.co.uk". web.archive.org. 2010-01-15. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-01-15. Iliwekwa mnamo 2022-08-02.
 9. "Kendrick Lamar & Black Hippy Sign To Aftermath & Interscope | Get The…". archive.ph. 2013-01-25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-01-25. Iliwekwa mnamo 2022-08-02.
 10. "Aftermath Entertainment", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-07-14, iliwekwa mnamo 2022-08-02
 11. Keith Nelson Jr (@JusAire) (2014-02-20). "50 Cent Leaves Interscope Records, New Album Coming June 3rd". AllHipHop (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-08-02.
 12. "Dr. Dre Announces New Album Compton: The Soundtrack, Explains Why Detox Never Came Out". Stereogum (kwa Kiingereza). 2015-08-01. Iliwekwa mnamo 2022-08-02.
 13. Peters, Mitchell (Januari 31, 2016). "Watch Dr. Dre Welcome Anderson .Paak to Aftermath Roster". Billboard. Iliwekwa mnamo Desemba 26, 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 14. Johnson, Elon; Parry, Heather (Oktoba 27, 2000). "Rakim Signs With Dr. Dre's Aftermath Records". MTV.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-03-08. Iliwekwa mnamo Desemba 26, 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 15. Caroline (Februari 20, 2014). "50 Cent And G-Unit Records Sign Exclusive Worldwide Distribution Agreement". PR Newswire. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Machi 3, 2014. Iliwekwa mnamo 2021-12-26.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 16. Kigezo:Cite magazine
 17. "Aftermath Music dot com | Dr. Dre Eminem 50 Cent Busta Rhymes Stat Quo Eve Bishop Lamont G.A.G.E." www.tenerifehotel.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Januari 22, 2011. Iliwekwa mnamo Novemba 5, 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 18. Reid, Shaheem (2009-12-09). "Timbaland Teams With Dr. Dre To Introduce Detroit MC Hayes - Music, Celebrity, Artist News". MTV. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-12-26. Iliwekwa mnamo 2021-12-26.
 19. Kigezo:Cite magazine
 20. Coleman, Lauren deLisa (Machi 24, 2017). "Here's How You Shake Up The Digital Content Game: Partner With Kanye West's Powerful, Secret Weapon". Forbes (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo Desemba 26, 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 21. Kigezo:Cite magazine
 22. "Taz Arnold: rocking his look and label, one at a time". Los Angeles Times. Januari 11, 2009. Iliwekwa mnamo Novemba 5, 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 23. "Taz Arnold: Your favorite producers favorite producer". Julai 14, 2010. Iliwekwa mnamo Novemba 5, 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aftermath Entertainment kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.