AZ (rapa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
AZ
AZ, mjini New York, mnamo 1998
AZ, mjini New York, mnamo 1998
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Anthony Cruz
Amezaliwa 5 Septemba 1972 (1972-09-05) (umri 51)
Asili yake East New York, Brooklyn, New York
Aina ya muziki Hip hop
Kazi yake MC, rapa
Miaka ya kazi 1992–mpaka sasa
Studio Virgin, Motown, Koch,
Tovuti www.doeordie2.com

Anthony Cruz (amezaliwa tar. 9 Mei 1972 mjini Brooklyn) ni rapa wa Kimarekani mwenye asili ya Dominika. anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama AZ. Pia, hujulikana zaidi na zaidi kwa kuwa rafiki mkubwa wa kitambo wa rapa mwenzi - Nas na kuwa mmoja kati ya wanachama wa kundi bab-kubwa la hip hop, The Firm, ikiwa ni pamoja na Nas, Nature na Foxy Brown. AZ anafahamika sana kwa maudhui yake ya uimbaji wa kina na silabasi mbalimbali.

AZ alianza kujipatia umaarufu baada ya kuonekana kwenye albamu ya Nas' ya Illmatic katika wimbo wa "Life's a Bitch" (1994)—tena alikuwa msanii mgeni pekee kuonekana kwenye albamu hiyo. Baada ya vita ya zabuni, AZ amesaini mkataba na EMI, na muda mfupi baadaye akatoa albamu ya Doe Or Die (1995) ikatamba sana, lakini ilipata mafanikio madogo kibiashara. Single kiongozi ya albamu, "Sugar Hill", imekuwa kibao pekee kupata mafanikio makubwa kibiashara kwa AZ akiwa kama msanii wa kujitegemea, kwa kufikia nafasi ya 25 kwenye chati za Billboard Hot 100, na kutunukiwa hadhi ya Gold. Mkataba wa AZ na EMI ulihamishiwa katika studio enzi ya Noo Trybe Records/Virgin Records wakati EMI Label Group imefungwa. Mnamo mwaka wa 1997, yeye na Nas wameonekana kwenye tangazo la biashara la Sprite . AZ akaingia mkataba na Motown/Universal Records na kutoa albamu ya 9 Lives.[1] Mnamo mwaka wa 2002, ametoa Aziatic. Single kutoka katika albamu, "The Essence," (akishirikiana na Nas) imepata kuchaguliwa kwenye ugawaji wa Tuzo za Grammy wa mara ya 45 kwa Ajili ya Rap Bora ya Wawili au Kundi.

Mnamo mwaka wa 2004, AZ alikuwa akipanga kutoa albamu - inge-kuwa albamu yake ya nne, Final Call, hata hivyo, lakini hatimaye ikatiwa kapuni kwa kufuatia kuvuja kwa ajabu na imetolewa kama Final Call (The Lost Tapes) mnamo 2008. Ametoa albamu zake za 4 na 5 A.W.O.L. na The Format mnamo 2005 na 2006, kwa pamoja. Halafu Undeniable ilitolewa mnamo 2008.

Na kwa mwezi wa Oktoba wa 2009, anafanyia kazi albamu yake yake ya 10 iitwayo Doe or Die 2 itakayotolewa mwanzoni mwa mwaka wa 2010.[2]. Ana matumaini ya kuwaingiza kikosi cha utayarishaji cha awali cha Doe Or Die kama vile L.E.S., Pete Rock, DR Period na Buckwild. Ametibitisha hata kwamba amefanya nyimbo mbili na Pete Rock, ikiwa ni pamoja na "Rather Unique Part II". AZ pia ana mpango wa kuchukua biti kutoka kwa DJ Toomp, Dr. Dre na Kanye West kwa ajili ya DOD2 ikiwa ni pamoja na kumwingiza mkali wake wa mistari wa zamani Nas, pia kwa mujibu wa akaunti yake kwenye Twitter ametaja ya kwamba ameomba biti kutoka kwa RZA vilevile na kupanga kuitoa albamu kunako mwezi wa Mei au Juni 2010.[3] Single ya kwanza kutoka albamu itakuwa "Feel My Pain" iliyotayarishwa na Frank Dukes.[4]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Albamu za studio[hariri | hariri chanzo]

Albamu za ushirika[hariri | hariri chanzo]

Kompilesheni albamu na Mixtapes[hariri | hariri chanzo]

Mionekano[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. allmusic Biography
  2. Davis, Meosha (2009-12-01). AZ: From Brooklyn to Hollywood. AllHipHop. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-01-04. Iliwekwa mnamo 2009-12-26.
  3. Arnold, Paul W (2009-12-22). AZ Wants Dr. Dre, Kanye West And Nas For Doe Or Die 2. HipHopDX. Iliwekwa mnamo 2009-12-26.
  4. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-03-01. Iliwekwa mnamo 2010-05-27.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

  • AZ katika MySpace