Nenda kwa yaliyomo

Friday

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Friday
Imeongozwa na F. Gary Gray
Imetayarishwa na Patricia Charbonnet
Imetungwa na Ice Cube
DJ Pooh
Nyota
Muziki na Frank Fitzpatrick
Simon Franglen
Chuck Wild
Imehaririwa na John Carter
Imesambazwa na New Line Cinema
Imetolewa tar. 26 Aprili 1995
Ina muda wa dk. Dakika 91
97 minutes (Director's cut)
Nchi Marekani
Lugha Kiingereza
Bajeti ya filamu $3.5 million
Mapato yote ya filamu $27.5 million

Friday ni filamu ya washikaji-ya-vichekesho ya mwaka wa 1995 kutoka nchini Marekani. Filamu imeongozwa na F. Gary Gray ikiwa ndiyo filamu yake ya kwanza kuongoza. Ndani yake anakuja Ice Cube, ambaye pia alishiriki katika kuandika muswaada andishi wa filamuna DJ Pooh, na Chris Tucker katika uhusika wake wa kwanza kwenye filamu. Filamu inaelezea masaa 16 ya maisha bila ajira ya Craig Jones (Cube) na Smokey (Tucker), ambaye anatakiwa alipe deni la dola 200 la mwuza dawa za kulevya ifikapo saa 4 kamili usiku huo.

Mafanikio ya filamu yamezaa matoleo mengine mawili: Next Friday (2000) na Friday After Next (2002). Sehemu ya nne ya filamu itaitwa Last Friday ilikuwa ikishuhulikiwa kwa miaka kadhaa sasa lakini imepitishwa mnamo mwezi wa Aprili 2017 - na hiyo ni kwa mujibu wa John Witherspoon.[1]

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Craig Jones (Ice Cube), bwana mdogo anayeishi mjini Los Angeles, amepoteza kazi yake hivi karibuni, baada ya kusingiziwa kwiba. Bila kuwa na mipango yoyote, anajiachia kibarazani kwao na mshikaji wake, Smokey (Chris Tucker), aliyejiachia, ambaye anauza dawa za kulevya kwa ajili ya Big Worm (Faizon Love), msambazaji wa dawa za kuelevya asiye na akili hata punje mtaani hapo.

Siku nzima, Craig na Smokey wanaangalia yanayojiri mtaani kwao. Wanakumbana na Ezail, ambaye anaunga mkono tabia zake za matumizi ya dawa za kulevya kwa viji-makosa; Debbie Parker (Nia Long), mwanamke mzuri ambaye Craig ana mahaba nae;jirani yake Craig, Stanley, ambaye mashauzi ya utajiri wake unamshangaza Craig; Red (DJ Pooh), mfanyakazi mwenzi wa zamani wa Craig na rafiki wa tangu utotoni ambaye baiskeli na kidani chake kiliporwa na Deebo (Tiny Lister Jr.), mkorofi wa mtaani; Mchungaji Clevor (Bernie Mac), mchungaji mtaani hapo, ambaye kabambwa akila uroda na mama wa Debbie Bib. Parker (Kathleen Bradley) mke wa Bwana Parker (Tony Cox); na Felisha, dada wa Debbie na demu wa Deebo, ambaye anamwudhi kila mtu mtaani kwao kwa tabia yake ya kuombaomba.

Smokey, ambaye alikuwa akivuta badala ya kuuza mibangi aliyopewa kuuza, ana mgogoro na Big Worm. Katika harakati zake za kutaka kujitetea upotevu wa pesa zake, Smokey anamsingizia Craig. Big Worm anatishia kuwaua wote iwapo hawatolipa pesa yake ifikapo saa nne kamili usiku.

Craig anakerekwa na kumvaa Smokey kuhusu ukosefu wake wa mipango ya kuuza bangi kabla ya kuamua kumsaidia Smokey. Craig anajaribu kuazima pesa kutoka kwa mamake Betty (Anna Maria Horsford) bila mafanikio; dada yake, Dana (Regina King); na demu wake mwenye wivu kichizi, Joi (Paula Jai Parker). Baba wa Craig, Willie (John Witherspoon), hatimaye anajua mpango wa Craig, vilevile habari ya Craig amebeba bunduki. Willie anaongea nae, na kumweleza ya kwamba Craig anapaswa kutumia mikono yake, badala ya bunduki, kwa kutatua matatizo yake, yote hayo alikuwa akimweleza Craig hadithi namna babake mdogo, ambaye ni ndugu wa Willie, alivyopoteza maisha akiwa na miaka 22 kwa fujo za matumizi ya bunduki.

Baadaye, wakati Craig na Smokey wanajadiliana juu ya hatma yao, wakaingiliwa na ujio wa Rita (Yvette Wilson), demu ambaye Debbie alimwunganishia mapema. Smokey anagundua ameongopa mwonekano wake: badala ya kufanana na Janet Jackson kama alivyodai hapo awali, Rita ni bonge halafu ana kipara.

Smokey anaelekea nyumbani kwa Debbie kulalamika, akiwa huko kaiona baiskeli ya Red katika kibustani. Kanyatia na kumkuta Deebo kalala na Felisha. Smokey anajaribu kuchukua pesa ambayo yeye na Deebo waliiba kwa Stanley mapema siku hiyo, lakini akavurugwa na Ezail. Wote wakatoroka bila pesa kabla Deebo kuamka. Smokey anarudi kwa kina Craig na kumwambia, na Craig anakubali kurudi tena akiwa na Smokey kwenda kujaribu tena, lakini kipindi hicho, Deebo anawapitia nyuma yao.

Wawili wale wanagundua kuna gari jeusi linapita na kujificha polepole, wanashuku huenda ikawa waendeshaji wanaotandika risasi. Wakaingia woga, wakakimbilia chumbani kwa Craig. Halafu, punde Willie anawavaa na suala la Big Worm, na muda wa saa usiku unakaribia, wanaamua kutoka nje. Wakiwa nje, wanagundua kuna gari dogo limeegesha mtaani huku taa zikiwa zimezimwa. Wawili hao wakachoropoka mbio kama wanaume wakielekea mahali gari lilipo huku wakitandika risasi upande ule.

Majirani wakatoka nje baada ya kusikia milio ya risasi ikilindima mtaani hapo. Debbie anamshambulia Deebo kwa kumchapa Felisha baada ya Deebo kwa kumsingizia Felisha jaribio la wizi wa Smokey. Deebo hatimaye anamshambulia Debbie, huku akina Craig na Smokey wakiwasili.

Imewakera kitendo cha Deebo kumtandika Debbie, Craig anasimama kiume kizichapa nae, na kumtishia kumtandika na bunduki. Deebo anapovuka na vitisho hivyo na Willie anamchochea Craig aweke bunduki chini na kupigana kwa mikono yake. Craig na Deebo wanalianzisha. Baada ya almanusura kushindwa, Craig anautafuta ushindi kwa kupigana hata vitu vingine kama silaha.

Wakati Debbie anamuinua Craig, Smokey anakwiba pesa kutoka kwa Deebo aliyezilai na kutoweka kutoka katika eneo la tukio. Red anampa za uso tena Deebo kuhakikisha haamki na kuchukua baiskeli na mnyororo wake huku Ezail akiiba viatu vya Deebo. Craig na Debbie wanakubaliana kukutana siku inayofuata huku Craig akivunja uhusiano wake na Joi kwa njia ya simu.

Baadayer, Smokey anayamaliza na Big Worm, na kumaliza uhasimu. Anatangaza kuacha uraibu wa dawa za kulevya na anaenda kufanya tiba. Baada ya kukata simu, Smokey anaangalia juu, anajinyoosha na filamu inaisha, huku akisema hivi kwa hadhira, "Nilikuwa nazingua tu'! Na unajua hili, eh!"

Washiriki[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. EURPublisher01. "John Witherspoon: Ice Cube Says New 'Friday' Movie Has Studio Greenlight". EURweb. Iliwekwa mnamo 2017-04-27.{{cite web}}: CS1 maint: numeric names: authors list (link)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: