Nenda kwa yaliyomo

DJ Pooh

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
DJ Pooh
Jina la kuzaliwaMark Jordan
Amezaliwa29 Juni 1969 (1969-06-29) (umri 55)
Los Angeles, California, United States
Kazi yakeMtayarishaji rekodi, rapper, mwigizaji wa sauti
Miaka ya kazi1984 - hadi sasa
Ameshirikiana naKing Tee, Chilly Chill, Kam, Ice Cube, Dr. Dre, Snoop Dogg

Mark Jordan (amezaliwa 29 Juni, 1969 mjini Los Angeles, California), anajulikana zaidi kwa jina lake la kisanii kama DJ Pooh ni mtayarishaji wa rekodi za muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani,[1]mwigizaji wa sauti, mghani, mwandishi muswaada andishi,[2] mwigizaji na mwongozaji wa filamu.[3][4] Anafahamika sana kwa uhusika wake kama "Red" katika filamu ya kwanza ya "Friday" ambayo alicheza na Ice Cube. DJ Pooh alishiriki kuandika "Friday" na alisaidia ujenzi wa wahusika katika filamu hiyo. Akiwa kama mkongwe wa kuchanganya madude katika muziki, amewahi kutayarisha albamu wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ice Cube, Del tha Funkee Homosapien, LL Cool J, Yo-Yo, Tha Dogg Pound , King Tee, na wengine kibao. Mwaka wa 1996, DJ Pooh alitoa msaada wa nguvu katika utayarishwaji wa albamu ya pili ya Snoop Dogg, Tha Doggfather. Albmu ilitunukiwa platinamu maradufu.

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
Taarifa za albamu
Bad Newz Travels Fast
  • Imetolewa: Julai 15, 1997
  • Nafasi za chati: #116 US, #34 Top R&B/Hip Hop
  • Tunukio la mwisho la RIAA: Hakuna
  • Single: "Whoop Whoop"

Filmografia

[hariri | hariri chanzo]
  • Last Friday kama (mwandishi mwenza)
  • Grow House kama Mwongozaji na Mwandishi
  • Friday kama Red (mwandishi mwenza)
  • The Wash kama Slim (Mwongozaji, mtayarishaji na mwandishi)
  • 3 Strikes kama Trick Turner/Taxi Driver (Mwongozaji na mwandishi)
  • The Boondocks kama Mudpie/Speaker #2/Crowd Member/Laughing Funeral Attendee (sauti tu)
  • Freaknik: The Musical kama Doela Man (sauti tu)
  1. [DJ Pooh katika Allmusic AllMusic ((( DJ Pooh > Overview )))
  2. DJ Pooh
  3. "Official website of Metro-Goldwyn-Mayer Inc. - Ars Gratia Artis". MGM.com. Iliwekwa mnamo 2017-04-18.
  4. By ELVIS MITCHELLNOV. 15, 2001 (2001-11-15). "FILM REVIEW; With Just a Hint of a Plot, Taking It Easy. Very Easy". New York Times. Iliwekwa mnamo 2017-04-18.{{cite web}}: CS1 maint: numeric names: authors list (link)

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]