Nenda kwa yaliyomo

Jason Statham

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jason Statham
Jason Statham
Jason Statham
Jina la kuzaliwa Jason Statham
Alizaliwa 26 Julai 1967
Uingereza
Kazi yake Mwigizaji
Mwanamitindo
Mwogeleaji

Jason Statham (amezaliwa 26 Julai 1967) ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Uingereza. Anafahamika zaidi kwa kucheza kama Bacon katika filamu ya Lock, Stock and Two Smoking Barrels, Jake Green katika filamu ya Revolver, Turkish katika filamu ya Snatch.

Pia Statham amepata kuonekana katika filmu nyingi sana za Kimarekani. Filamu hizo ni kama vile The Italian Job, Crank, The One na War ambazo zote alicheza na miwgizaji filamu mashuhuri wa Kichina Jet Li. Vilevile katika The Transporter, humo alicheza kama nyota kiongozi wa filamu hiyo na inaamika kwamba ile ndiyo iliyomfanya aonekane zaidi kwa watu wa Marekani.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Statham alizaliwa mjini [Shirebrook], Derbyshire na baadaye kuhamia mjini London. Ni mtoto wa pili wa wazazi ambao mmoja wao alikuwa mwimbaji na mwingine mwundaji wa nguo. Alikulia katika maisha ya kimichezo na ni mwogeleaji mzuri - mwanariadha. Na amewahi kushinda mashindano ya kimataifa ya mbio kwa mwaka wa 1992.[1] Vilevile amewahi kuwa mwanachama wa Kikosi cha Waogeleaji cha Taifa cha Britain kwa takriban miaka kumi na miwili. Pia Statham ni mtaalam wa martial arts na Kick Boxing.

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Statham amewahi kuwa mahusiano ya kimapenzi na mwigizaji filamu-mwanamitindo wa Kiingereza Bi. Kelly Brook kwa takriban miaka saba, lakini wakaja kutengana pale mwanamama Kelly alipokutana na mwigizaji filamu mwenzi Bw. Billy Zane wakati wa kucheza filamu ya Survival Island na kupelekea kuwa mpenzi wa mwigizaji huyo. Mnamo mwaka wa [2005], Statham akaanzisha mahusiano na mwimbaji wa zamani Bi. Sophie Monk, lakini mapenzi yao hayakudumu sana wakaachana.

Filamu alizocheza

[hariri | hariri chanzo]
MwakaJina la filamuJina alilotumiaMaelezo
1998Lock, Stock and Two Smoking BarrelsBacon
2000SnatchTurkish
Turn It UpMr. B
2001Ghosts of MarsSgt. Jericho Butler
The OneMVA Agent Evan Funsch
Mean MachineMonk
2002Thai Boxing: A Fighting ChanceNarrator
The TransporterFrank Martin
2003The Italian JobHandsome Rob
2004CollateralAirport ManCameo appearance
CellularEthan Greer
2005Transporter 2Frank Martin
RevolverJake Green
LondonBateman
2006ChaosDetective Quentin Conners
The Pink PantherYves GluantUncredited role
CrankChev Chelios
2007WarFBI Agent John Crawford
In the Name of the King: A Dungeon Siege TaleFarmer Daimon
2008The Bank JobTerry Leather
Death RaceFrankensteinawaiting release
2009Transporter 3Frank Martinfilming
Crank 2: High VoltageChev Cheliosfilming

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: