Nenda kwa yaliyomo

Charlize Theron

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Charlize Theron

Charlize Theron akiwa kwenye sherehe ya 2015 Cannes Film Festival
Amezaliwa Charlize Theron
Benoni
Afrika Kusini
Miaka ya kazi 1995 – hadi sasa
Tovuti rasmi

Charlize Theron (amezaliwa Benoni, Gauteng, Afrika Kusini, 7 Agosti 1975) ni mwigizaji wa filamu na mwanamitindo wa zamani wa Kiafrika Kusini-Kimarekani. Huenda akawa anafahamika kwa jina la Stella Bridger kutoka katika filamu ya The Italian Job, Aileen Wuornos kutoka katika filamu ya Monster, ambayo ilimwezesha kujipatia Tuzo ya Academy.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Theron baba yake ni Charles Theron, aliyekuwa mmiliki wa Kampuni ya Ujenzi yenye asili kamili ya Ufaransa. Mama yake, Gerda, mwenye asili ya Kijerumani, akaja kushikilia madaraka baada ya kifo cha mumewe. Theron lugha yake ya kwanza ni Kiafrikaans. Pia ni mwongeaji wa Kiingereza fasaha na Xhosa.

Theron alikulia katika mazingira ya kuwa mtoto pekee wa familia hiyo iliyokuwa ikiishi shamba karibu kidogo na mji wa Johannesburg katika kitongoji cha Benoni. Akiwa na umri wa miaka kumi na tatu,Theron alipelekwa kwenda kusoma katika shule ya bweni (National School Of The Arts) ya mjini Johannesburg.

Akiwa na umri wa miaka kumi na tano, Theron alishuhudia kifo cha baba yake, kilichosababishwa na pombe, yani mamake alimtwanga risasi mumewe kwa bahati mbaya pale alipotaka kujaribu kujilinda mwenyewe dhidi ya mashambulizi aliyokuwa akiyatoa mumwe. Hakuna hukumu yoyote iliyopitishwa juu ya hilo na badala yake mama wa Theron akaachiwa huru.

Baadhi ya filamu alizocheza Theron[hariri | hariri chanzo]

 • 1995 - Children of the Corn III: Urban Harvest
 • 1996 - 2 Days in the Valley
 • 1996 - That Thing You Do!
 • 1997 - Trial and Error
 • 1997 - The Devil's Advocate
 • 1998 - Celebrity
 • 1998 - Mighty Joe Young
 • 1999 - The Astronaut's Wife
 • 1999 - The Cider House Rules
 • 2000 - Reindeer Games
 • 2000 - The Yards
 • 2000 - The Legend of Bagger Vance
 • 2000 - Men of Honor
 • 2001 - Sweet November
 • 2001 - The Curse of the Jade Scorpion
 • 2001 - 15 Minutes
 • 2002 - Trapped
 • 2002 - Waking Up in Reno
 • 2003 - The Italian Job
 • 2003 - Monster
 • 2004 - The Life and Death of Peter Sellers
 • 2004 - Head in the Clouds
 • 2005 - North Country
 • 2005 - Æon Flux
 • 2007 - In the Valley of Elah
 • 2007 - Battle in Seattle
 • 2008 - Sleepwalking

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons