Nenda kwa yaliyomo

R. Kelly

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
R. Kelly

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Robert Sylvester Kelly
Amezaliwa 8 Januari 1967 (1967-01-08) (umri 57)
Chicago, Illinois, Marekani
Aina ya muziki R&B, soul, pop
Kazi yake Mwimbaji-mtunzi-wa-nyimbo, rapa, mwanamuziki, mtayarishaji wa rekodi, mtayarishaji mtendaji, mtendaji wa rekodi, mpiga vyombo vingi-vingi, mwongozaji wa muziki wa video
Ala Sauti, piano, kinanda
Miaka ya kazi 1986–mpaka sasa
Studio RCA/Jive Label Group/Zomba Label Group/Sony Music Entertainment (1990–esent)
Blackground Records (1993–05)
Tovuti www.r-kelly.com


Robert Sylvester Kelly (amezaliwa tar. 8 Januari 1967) ni mwimbaji wa muziki wa R&B na soul-mtunzi wa nyimbo, rapa, na mtayarishaji wa rekodi kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama R. Kelly. Alianza kuingia katika kazi ya muziki kwa mara kwanza kunako mwaka wa 1992 akiwa na kundi la Public Announcement, halafu baadaye Kelly akaenda kuwa kama msanii wa kujitegemea mnamo 1993 na kuweza kupata mafanikio makubwa kabisa kwa kazi za kujitegemea baada ya kutoa albamu yake ya 12 Play.

Kelly alifahamika sana kwa mkusanyiko wa vibao vyake vikali kama vile "Bump n' Grind", "I Believe I Can Fly", "Gotham City", "Ignition", "If I Could Turn Back the Hands of Time", "The World's Greatest", na hip-hopera ya "Trapped in the Closet".

Kelly pia ametayarisha na kuimba katika nyimbo nyingine kibao za wasanii wengine wa R&B na hip-hop. Mnamo mwaka wa 1994, Kelly ametayarisha na kutunga albamu ya kwanza ya mwimbaji wa R&B Aaliyah na mwaka wa 1995, Kelly ameshiriki-kutayarisha na kutunga wimbo wa "You Are Not Alone" kwa ajili ya Michael Jackson, ambao uliingizwa kwenye albamu ya Jackson, HIStory.

Kelly ameimba viitikio vya nyimbo kibao maarufu za hip-hop. Nyimbo ni pamoja na "Fuckin' You Tonight" ya The Notorious B.I.G., "We Thuggin'" ya Fat Joe, "Gigolo" ya Nick Cannon, na "Go Getta" ya Young Jeezy, na ameshirikiana na Jay-Z katika albamu mbili za pamoja.

Katika maisha yake binafsi, Kelly amekuwa na kashfa kadhaa za ngono. Taarifa zilielezwa kwamba amemwoa kabinti kadogo Aaliyah, ambaye yeye ndiye alikuwa mtunzi wake wa nyimbo. Kelly na Aaliyah wakasitisha ndoa yao. Baada ya kutolewa video ya mtu moja aliyedaiwa kuwa yeye kufanya mapenzi na msichana mdogo, Kelly akashtakiwa katika kesi kadhaa za ngono za watoto mnamo 2002.[1] Baada ya makawio kadhaa, kesi yake ikapelekwa kizimbani mnamo 2008, na baraza la wazee wa mahakama likamwona Kelly hana kosa katika mshtaka yote 14.[2]

Januari 2019 kipindi cha televisheni cha Lifetime kilitoa filamu fupi iitwayo Surviving R. Kelly iliyoonyesha wanawake wanaomshutumi kwa unyanyasaji wa kingono. Kutokana na tuhuma hizo, kampuni ya RCA Records ilufuta mkataba wake na Kelly.[3] Februari 22, 2019, Kelly alifunguliwa mashtaka mengine 10.[4] Julai 11, 2019, Kelly alikamatwa kwa mashataka kadhaa ya ngono.[5] [6] Hadi Julai 12, 2019, Kelly anakabiliana na mashtaka 18 ikiwa ni pamoja na kufanya mapenzi na watoto wadogo, kuteka nyara na kazi ya kulazimishwa. [7]

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]

Filmografia

[hariri | hariri chanzo]
 • 2005: Trapped in the Closet (1–)
 • 2007: Trapped in the Closet (13–)
 • 2007: R. Kelly Live The Light It Up Tour
 • Billboard Awards
  • 2001: Top R&B/Hip Hop Artist
  • 2001: Top R&B/Hip Hop Album (TP2.com)
  • 2001: Top R&B/Hip Hop Singles & Tracks (“Fiesta”)
  • 2001: Top R&B/Hip Hop Artist –ale
  • 2001: Top R&B/Hip Hop Album Artist
  • 2001: Top R&B/Hip Hop Album Artist –ale
 • BMI Awards
  • 1998: Mwimbaji na Mtunzi Bora wa Pop wa Mwaka (kwa ajili ya “I Believe I can Fly”, “I Can’t Sleep Baby (If I)”, na “I Don’t Want To” (imerekodiwa na Toni Braxton)
 • Grammy
  • 1998: Wimbo Bora wa R&B ("I Believe I Can Fly")
  • 1998: Mwimbaji Bora wa Kiume wa R&B ("I Believe I Can Fly")
  • 1998: Wimbo Bora Halisi wa Kibwagizo cha Filamu ("I Believe I Can Fly")
 • NAACP Image Awards
  • 2001: Outstanding Male Artist
  • 2001: Outstanding Music Video (“I Wish”)
 • Soul Train Awards
  • 1999: Best R&B/Soul Album, Male (R.)
  • 1999: Sammy Davis Jr. Entertainer of the Year Award
  • 2000: Best R&B/Soul or Rap Album (R.)
  • 2001: Best R&B/Soul Single, Male (“I Wish”)
  • 2001: Best R&B/Soul Album, Male (TP2.com)
  • 2004: R&B/Soul Album, Male (“Chocolate Factory”)
  • 2004: Quincy Jones Award for Outstanding Career Achievements
  • 2006: Stevie Wonder Award for Outstanding Achievements in Song Writing
 • Source Hip Hop Awards
  • 1999: R&B Artist of the Year
  • 2001: R&B Artist of the Year
 1. W. Fountain, John. "R. Kelly, R & B Star, Is Indicted on Child Sex Charges", The New York Times, June 6, 2002. 
 2. Streitfeld, David. "R. Kelly Is Acquitted in Child Pornography Case", The New York Times, June 14, 2008. 
 3. Aswad, Jem; Aswad, Jem (Januari 18, 2019). "R. Kelly Dropped by Sony Music". Variety. Iliwekwa mnamo Januari 18, 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 4. "R Kelly 'charged with sexual offences'", 22 February 2019. Retrieved on 22 February 2019. 
 5. "R. Kelly arrested in Chicago after being indicted by federal grand jury on new sex crime charges", Chicago Tribune, July 11, 2019.
 6. https://www.nytimes.com/2019/07/12/nyregion/rkelly-arrested.html
 7. "R. Kelly Arrested On Federal Charges, Including Child Pornography And Kidnapping". NPR.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-07-13.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu R. Kelly kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.