Bump n' Grind
“Bump n' Grind” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya R. Kelly kutoka katika albamu ya 12 Play | |||||
Imetolewa | 15 Januari 1994 | ||||
Muundo | CD single, Cassette single, 7" vinyl | ||||
Imerekodiwa | 1993 | ||||
Aina | R&B | ||||
Urefu | 4:16 | ||||
Studio | Jive Records | ||||
Mtunzi | R. Kelly | ||||
Mtayarishaji | R. Kelly | ||||
Mwenendo wa single za R. Kelly | |||||
|
"Bump n' Grind" ni wimbo ulioandikwa, kutayarishwa na kuimbwa na mwanamuziki wa R&B R. Kelly. Ilikuwa single ya pili kutolewa katika albamu yake ya kwanza akiwa kama msanii wa kujitegemea ya 12 Play mnamo 1994. Wimbo umepata kuwa wimbo pekee wa Kelly kushika namba moja nchini Marekani kwenye chati za Billboard Hot 100 (ikaingilia kati kwa muda kibao kilichokaa majuma sita cha Ace of Base cha "The Sign") akiwa kama msanii wa kujitegemea, pia ikapata kutumia majuma kumi na mawili ikiwa kama namba moja kwenye chati za Marekani, Hot R&B Songs, na kuufanya kuwa wimbo uliotamba kwa muda mrefu sana ukiwa kama wimbo namba moja wa R&B nchini Marekani kwa kipindi hicho. Wimbo pia umepata kushika namba nane kwenye chati za Ufalme wa Muungano, kupelekea mafanikio makubwa kabisa ya single yake iliyopitwa, "She's Got That Vibe" (ambayo kiukweli ilitolewa upya).
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bump n' Grind kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |