Eustasi White

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Eustasi White (Louth, Uingereza, 1559London, 10 Desemba 1591) alikuwa Mkristo wa Kanisa la Anglikana kabla hajajiunga na Kanisa Katoliki.

Baada ya kuhamia Ulaya bara, aliingia seminari kwa lengo la kurudi kwao kufanya uchungaji usioruhusiwa na serikali, akapewa daraja ya upadri (1588).

Hapo alirudi Uingereza lakini baada ya muda mfupi aliuawa kwa kunyongwa na kukatwa vipandevipande chini ya sheria.

Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39.

Sikukuu yake ni tarehe ya kifodini chake[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.