Europi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Europium)


Europi
Jina la Elementi Europi
Alama Eu
Namba atomia 63
Mfululizo safu Lanthanidi
Uzani atomia 151.964
Valensi 2, 8, 18, 25, 8, 2
Densiti 5.264
Kiwango cha kuyeyuka °K 1099
Kiwango cha kuchemka °K 1802
Hali maada mango

Europi (Europium) ni elementi ya kikemia yenye alama Eu na namba atomia 63, maana yake kuna protoni 63 katika atomu. Europi imepangwa kwenye jedwali la elementi katika kundi la lanthanidi. Ni elementi inayotendana haraka sana na hewa au unyevu, hivyo inahitaji kutunzwa ndani ya viowevu visivyotendana nayo.

Europi ni metali laini sana: inaweza kukatwa kwa kisu. Kama haikuoksidika rangi yake ni nyeupe ya kung'aa.

Ilisafishwa mara ya kwanza kwenye mwaka 1901 ikapewa jina la bara la Ulaya (Europa). [1]

Matumizi ya europi hutumia tabia ya mmemetuko (phosphorescence) wa kampaundi zake. Ni elementi adimu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Periodic Table: Europium". Royal Society of Chemistry. 

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Europi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.