Eleazari
Mandhari
Eleazari (kwa Kiebrania: אֶלְעָזָר, ʼElʽazar au ʼElʽāzār; maana yake "Mungu amesaidia") alikuwa kuhani mkuu wa pili katika Biblia ya Kiebrania baada ya kifo cha baba yake Aroni[1], kaka wa Musa.
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Septemba au 30 Julai[2].
Wengine walioitwa Eleazari katika Biblia
[hariri | hariri chanzo]Wanaume wengine sita wanatajwa kwa jina hilo katika Biblia:
- Eleazari bin Aminadab, aliyetunza Sanduku la Agano
- Eleazari bin Dodo, shujaa wa Mfalme Daudi
- Eleazari bin Pinhas, aliyetunza vyombo vitakatifu vilivyorudishwa Yerusalemu baada ya Uhamisho wa Babeli
- Eleazari Avaran, aliyeua tembo vitani
- Eleazari mfiadini, aliyeuawa katika dhuluma ya Antioko IV Epifane
- Eleazari bin Eliudi, baba mzaa babu wa Yosefu (mume wa Maria).
Jina hilo liliandikwa kwa Kigiriki "Lazaro", kama kwa rafiki wa Yesu Lazaro wa Bethania.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Hesabu 20:26-28
- ↑ https://catholicsaints.info/eleazar-the-patriarch/
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Eleazari kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |