Dmitri Bondarenko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dmitri Mikhailovich Bondarenko (kwa Kirusi Дмитрий Михайлович Бондаренко; amezaliwa Moscow tarehe 9 Juni 1968) ni mtaalamu wa historia ya Afrika na mwanaanthropolojia wa kijamii toka Urusi. Yeye ni daktari wa historia (2000), profesa (2007) na mwanachama wa Chuo cha Sayansi cha Urusi (2016), mwanasayansi mwandamizi na naibu mkurugenzi wa Taasisi ya Afrika ya Chuo cha Sayansi cha Urusi, profesa wa Chuo Kikuu cha Urusi cha Elimu Utu anayeongoza pia Kituo cha Kimataifa cha Anthropolojia cha Chuo Kikuu cha Uchumi. Mbali na hayo Bw. Bondarenko ni mwanzilishi na mhariri mwenza wa jarida la kimataifa la Maendeleo ya Kijamii na Historia (Social Evolution and History)[1].

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1990 alihitimu kwa heshima katika Idara ya Ethnografia ya Kitivo cha Historia cha Chuo Kikuu cha Moscow. Mwaka 1993 alipata digrii ya uzamivu wa historia akitetea tasnifu ambayo mada yake ni Jamii ya Ufalme wa Benin kabla ya mahusiano na Wazungu na vipengele vyake vya ngazi na ustaarabu[2].

Kuanzia Agosti mwaka 1990 anafanya kazi katika Taasisi ya Afrika. Tangu Aprili 2008 yeye ni naibu mkurugenzi wa shughuli za kisayansi na kuanzia Machi mwaka 2018 ana cheo cha mwanasayansi mwandamizi. Vile vile anaratibu kazi ya Kituo cha Uchunguzi wa Nchi za Afrika kusini mwa Sahara, Kituo cha Historia na Anthropolojia ya Kitamaduni pamoja na Kituo cha Uchunguzi wa Elimujamii na Siasa cha Taasisi hiyo.

Tangu Septemba mwaka 1996 anafundisha katika Chuo Kikuu cha Urusi cha Elimu Utu. Huko mwaka 2000 alitetea tasnifu ya udaktari kuhusu historia ya Benin kabla ya zama za ufalme, ujenzi na maendeleo ya muundo wake wa kijamii na kisiasa.

Anaongoza Kituo cha Kimataifa cha Anthropolojia cha Chuo Kikuu cha Uchumi tangu kuanzishwa kwake mnamo Februari mwaka 2018.

Alialikwa kufanya kazi katika Chuo Kikuu cha Evanston nchini Marekani (miaka 1993-1994), Taasisi ya Historia ya Jumuiya ya Max Planck mjini Göttingen huko Ujerumani (miaka 2003 na 2006) na Jumba la Elimu Utu mjini Paris, Ufaransa (mwaka 2005).

Miaka ya 1990-2010 aliwahi kuwa mhadhiri kwenye Vyuo Vikuu vya Angola, Misri, Urusi, Marekani, Slovenia, Tanzania na Uganda. Pamoja na hayo Dmitri Bondarenko ni mwanchama wa Jumuiya ya Anthropolojia ya Marekani, Jumuiya ya Wanaanthropolojia na Wanaethnografia wa Urusi (kama mjumbe wa Kamati ya Utendaji na mwenyekiti wa Tume ya Anthropolojia ya Siasa), Jumuiya ya Utafiti wa Afrika ya Marekani, Jumuiya ya Uchunguzi wa Afrika ya Australasia na Oceania, Shirika la Wanaanthropolojia wa Kijamii wa Ulaya (kama kiongozi wa kundi la wataalamu wa Afrika miaka 2006-2008), Umoja wa Kimataifa wa Elimu za Anthropolojia na Ethnografia, Jamii ya Wataalamu wa Afrika ya Ufaransa na Jamii ya Utafiti wa Maendeleo ya Kitamaduni.

Aliongoza utafiti wa shambani wa wataalamu wa Urusi katika nchi za Afrika kama vile Tanzania (miaka 2003, 2005, 2007), Nigeria (2006), Benin (2008), Rwanda (2009), Zambia (2010), Uganda (miaka 2017 na 2018) na pia kati ya Waafrika nchini Urusi (2007-2016) na Wamarekani weusi (miaka 2013-2015 na 2022).

Yeye yupo katika Tume Kuu ya Kutathmini ya Shirikisho la Urusi. Tangu tarehe 28 Oktoba 2016 yeye ni mwanachama wa Idara ya Taaluma za Historia, Fasihi na Lugha ya Chuo cha Sayansi cha Urusi.

Alisifiwa na Robert L. Carneiro na Henri J. M. Claessen[3][4].

Fani yake[hariri | hariri chanzo]

Maandishi[hariri | hariri chanzo]

Aliandika zaidi ya vitabu 8 vya kisayansi vikiwemo 5 vilivyochapishwa kwa Kiingereza:

Baadhi ya makala zake ni:

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Journal «Social Evolution & History»". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-05-17. Iliwekwa mnamo 2010-11-01.  Unknown parameter |deadlink= ignored (|dead-url= suggested) (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help)Jalada kutoka juu ya 2019-05-17. Iliwekwa mnamo 2010-11-01.
  2. "Постановления Президиума РАН". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-01-30. Iliwekwa mnamo 2016-01-07.  Unknown parameter |deadlink= ignored (|dead-url= suggested) (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help)Jalada kutoka juu ya 2016-01-30. Iliwekwa mnamo 2016-01-07.
  3. "In Memoriam: Robert L. Carneiro (1927-2020)". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-04-25. Iliwekwa mnamo 2022-05-27.  Unknown parameter |deadlink= ignored (|dead-url= suggested) (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help)Jalada kutoka juu ya 2022-04-25. Iliwekwa mnamo 2022-05-27.
  4. "Some Reminiscences about Henri J. M. Claessen". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-06-04. Iliwekwa mnamo 2023-12-07.  Unknown parameter |deadlink= ignored (|dead-url= suggested) (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help)Jalada kutoka juu ya 2023-06-04. Iliwekwa mnamo 2023-12-07.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]