Nenda kwa yaliyomo

Lemuri Kibete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Cheirogaleus)
Lemuri kibete
Lemuri kibete mkubwa
Lemuri kibete mkubwa
Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Eukaryota (Viumbe walio na seli zenye kiini)
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Primates (Wanyama wanaofanana kiasi na binadamu)
Nusuoda: Strepsirrhini (Wanyama wanaofanana zaidi na lemuri)
Oda ya chini: Lemuriformes (Wanyama kama kima)
Familia ya juu: Lemuroidea (Lemuri)
Familia: Cheirogaleidae (Lemuri walio na mnasaba na lemuri kibete)
Jenasi: Cheirogaleus
E. Geoffroy, 1812
Ngazi za chini

Spishi 5:

Lemuri kibete (kutoka Kiingereza: dwarf lemur) ni spishi za lemuri wa jenasi Cheirogaleus katika familia Cheirogaleidae. Kama lemuri wote wanatokea Madagaska tu. Lemuri hawa ni wakubwa kuliko lemuri-panya lakini wadogo kuliko lemuri wote wengine. Urefu jumla, pamoja na mkia, ni sm 35-45. Huenda katika matabaka ya chini ya uoto wa misitu ya Madagaska ya Mashariki. Hula matunda na maua hasa na husaidia uchavushaji wa mimea fulani. Wakati wa majira ya baridi hulala kwa kiwewe katika matundu ya miti kwa muda wa miezi minne hadi mitano. Hudunduliza mafuta katika sehemu ya mkia wanayoyatumia wakati wa vipindi vya upungufu wa chakula.

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.