Nenda kwa yaliyomo

Mwanaidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bi. Mwanaidi)
Mwanaidi
muhusika wa Siri ya Mtungi

Taswira ya Mwanaidi (uhusika umechezwa na Betty Kazimbaya)
Imebuniwa na MFDI Tanzania
Imechezwa na Betty Kazimbaya
Misimu
1, 2
Maelezo
Jinsia Kike
Kazi yake Mama wa nyumba
Mfanyabiashara
Familia Mzee Kizito
Ndoa Mzee Kizito
Watoto Shoti
Cheusi Mtungi
Dini Mwislamu
Utaifa Mtanzania

Mwanaidi ni jina la uhusika kutoka katika tamthilia ya Siri ya Mtungi kutoka nchini Tanzania. Uhusika umechezwa na Betty Kazimbaya. Huyu ni mke wa pili wa Mzee Kizito, baada ya Farida na Vingawaje - kabla ya ujio wa Nusura. Katika tamthilia yote ya Siri ya Mtungi, mtu ambaye ameonesha busara ya hali ya juu ni Mwanaidi. Mama mzazi wa Cheusi na mlezi wa Shoti na Sabrina. Mfanyabiashara na mama wa nyumbani. Ana karakana yake ya kuandaa unga wa mahindi na kuuza. Vilevile ndiye mke pekee anayefuatwa kwa ushauri mara kwa mara na Mzee Kizito.

Ni mama asiyependa kuona familia yake inayumba. Tena ana thubutu hata kumkanya mwanae asiendekeze tabia ya kuzaa-zaa kila wakati. Hali ambayo itamfanya achoke mapema. Yeye aliweza kujizuia zamani, na ndiyo maana anaonekana bado kijana. Hekima na busara, hapa ndio nyumbani kwake.

Kama ilivyo kwa wanadamu wote, hakuna aliyemkamilifu. Mwishoni mwa msimu wa pili, Mwanaidi, alionekana kuwa na mchepuko kamwingiza nyumbani kwa mumewe. Alifumwa na Cheusi wakati anatafuta khanga ya kumsitiri mtoto wake. Jambo hili lilimuumiza sana Cheusi. Tangu hapa hakuwa tayari tena kuchukua ushauri juu ya uhusiano katika ndoa yake. Kama yake mama mmeshinda, ya Cheusi ataiweza. Tukio hili lilimfanya Cheusi akae chini na mumewe ili wapange familia yao kwa namna ambavyo wao wanataka na si kuendeshwa tena na mtu yeyote yule.

Pamoja na yote, Mwanaidi ana moyo wa upendo kwa wake wenzake wote. Licha ya Farida kuonesha kutokubaliana na kila jambo kutoka wake wenzake. Mwanaidi ndiye aliyempeleka hospitali Nusura pindi alipojisikia kujifungua na vilevile aliwahi kumsindikiza hospitali. Hakumnyanyapaa baada ya kusikia Nusura ana UKIMWI. Na baada ya Kizito kuonekana hana tena maambukizi, Mwanaidi akaona heri awe mpweke kuliko kuishi maisha ya mitala ambayo mwisho wake ulikuwa ni kuambikizwa tu maradhi.

Hadi msimu wa pili unaisha, Mwanaidi na Mzee Kizito walibaki kuwa wazazi tu, licha ya Kizito kubembeleza sana. Mara ya mwisho walikutana katika tamasha la Taarab lililokuwa limeandaliwa na bendi ya taarab ambayo Sabrina anaiimbia.

[1]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Mwanaidi Ilihifadhiwa 12 Septemba 2016 kwenye Wayback Machine. katika wavuti rasmi ya Siri ya Mtungi.