Nenda kwa yaliyomo

Kovu (Siri ya Mtungi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kovu
muhusika wa Siri ya Mtungi

Taswira ya Kovu (Siri ya Mtungi) (uhusika umechezwa na Khalidi Nyanza)
Imebuniwa na MFDI Tanzania
Imechezwa na Khalidi Nyanza
Misimu
1, 2
Maelezo
Jinsia Kiume
Kazi yake Tapeli, mpiga dili, jambazi
Utaifa Mtanzania

Kovu ni jina la uhusika kutoka katika tamthilia ya Siri ya Mtungi kutoka nchini Tanzania. Uhusika umechezwa na Khalidi Nyanza. Huyu ni kijana mdogo anajiyehusisha na vitendo vya kijambazi na uingizwaji wa mali za magendo kupitia pwani. Awali alionekana akimpatia Duma mizigo ya wizi akauze na baadaye kujenga urafiki - mwishowe uadui akimtumikia jangili kuu Mzee Masharubu. Kovu ni askari mwaminifu sana kwa Masharubu. Alikuwa anapeleka umbea kwa Masharubu kuhusu Duma na kazi zake magendo kutoka kwa wasambazaji wengine, hali ambayo ilileta mgongano mkubwa wa kimaslahi na hatimaye Duma na Golden (rafiki mpya wa Duma na mnasihi wa dawa za kulevya chini ya Zungu la Unga Ish) kuuawa na Kovu.[1]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Kovu (Siri ya Mtungi) Archived 21 Desemba 2019 at the Wayback Machine. katika wavuti rasmi ya Siri ya Mtungi.