Nenda kwa yaliyomo

Cheusi Mtungi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Cheusi Mtungi
muhusika wa Siri ya Mtungi

Taswira ya Cheusi Mtungi (uhusika umechezwa na Godliver Gordian
Imebuniwa na MFDI Tanzania
Imechezwa na Godliver Gordian
Misimu
1, 2
Maelezo
Jinsia Kike
Kazi yake Mama wa nyumbani
Ndoa Cheche Mtungi
Watoto 3
Ndugu Shoti
Dini Mwislamu
Utaifa Mtanzania

Cheusi Mtungi ni jina la uhusika kutoka katika tamthilia ya Siri ya Mtungi kutoka nchini Tanzania. Uhusika umechezwa na Godliver Gordian. Cheusi ni mke halali wa Cheche Mtungi. Anapitia magumu mengi kwenye ndoa yake lakini anayatatua kwa aina yake. Sifa kuu ya Cheusi ni uvumilivu wake katika ndoa - hasa ukizingatia mumewe ni mtu wa wanawake sana. Sifa nyengine aliyonayo ni pamoja na upole na unyenyekevu kwa mume na mama yake mzazi Bi. Mwanaidi. Hapendi kuyumbishwa kwa ndoa yake na mtu yeyote yule hata kama ni mama yake mzazi ndiye myumbishaji.[1] Kwa upande wa familia aliyozaliwa, yeye ni mtoto wa kwanza wa Bi. Mwanaidi ambaye ni mke wa pili wa Mzee Kizito. Cheusi ni dada wa Shoti, ambaye anaonekana kidogo kuwa na kautahira.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Cheusi Mtungi Archived 12 Septemba 2016 at the Wayback Machine. katika wavuti rasmi ya Siri ya Mtungi.