Mzee Masharubu
Mandhari
(Elekezwa kutoka Masharubu)
Masharubu | |
---|---|
muhusika wa Siri ya Mtungi | |
Taswira ya Mzee Masharubu (uhusika umechezwa na MacDonald Haule) | |
Imebuniwa na | MFDI Tanzania |
Imechezwa na | MacDonald Haule |
Misimu | 1, 2 |
Maelezo | |
Jinsia | Kiume |
Kazi yake | Tapeli, dhulmati, jangili, mpiga dili |
Utaifa | Mtanzania |
Mzee Masharubu ni jina la uhusika kutoka katika tamthilia ya Siri ya Mtungi kutoka nchini Tanzania. Uhusika umechezwa na MacDonald Haule. Huyu ni baba mzazi wa Nusura. Mtu mmoja dhulmati sana. Maisha yake karibia yote ya kunjunga na kuumiza wengine. Mtu asiyefaa katika jamii. Madili ya mjini, hayamwachi kando. Ana njia zake za kuingiza mizigo ya magendo. Amekuwa akipapurana sana na Duma katika biashara zake hadi kupelekea mauti yake. Vilevile alikuwa mwenye nyumba katika banda ambalo Duma alipanga. Jitu la kunyanyasa watu na asiye na huruma hata kwa mwanawe.[1]
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Mzee Masharubu Ilihifadhiwa 21 Desemba 2019 kwenye Wayback Machine. katika wavuti rasmi ya Siri ya Mtungi.