Farida

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bi. Farida)
Farida
muhusika wa Siri ya Mtungi

Taswira ya Farida (uhusika umechezwa na Halima Maulid)
Imebuniwa na MFDI Tanzania
Imechezwa na Halima Maulid
Misimu
1, 2
Maelezo
Jinsia Kike
Kazi yake Mama wa nyumba
Familia Mzee Kizito
Ndoa Mzee Kizito
Dini Mwislamu
Utaifa Mtanzania

Farida ni jina la uhusika kutoka katika tamthilia ya Siri ya Mtungi kutoka nchini Tanzania. Uhusika umechezwa na Halima Maulid. Huyu ni mke wa kwanza wa Mzee Kizito. Mama mwenye choyo na kila mja. Hapendi maendeleo ya wenzie na mwingi wa ushirikina. Kumekuwa na malalamiko mengi kwa kila mke aliyeolewa na Mzee Kizito. Fununu zinaeleza kuwa yeye ndiye aliyemuua kwa uchawi mke wa tatu wa Kizito, Vingawaje. Tangu msimu wa kwanza hadi wa pili, hakuna mahali alipoonesha furaha. Maisha ya Bi. Farida yamejawa na choyo na roho mbaya. Hakupata elimu yoyote ile maishani hasa ukizingatia aliolewa akiwa bado yungali binti mdogo kabisa. Ndoa za miaka ya zamani. Hana hofu ya Mungu wala mwanadamu mwengine yeyote yule. Mshirikina hakuna mfano. [1]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Farida Archived 12 Septemba 2016 at the Wayback Machine. katika wavuti rasmi ya Siri ya Mtungi.