Sabrina Kizito

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sabrina
muhusika wa Siri ya Mtungi

Taswira ya Sabrina Kizito (uhusika umechezwa na Patricia Nyamaka)
Imebuniwa na MFDI Tanzania
Imechezwa na Patricia Nyamaka
Misimu
1, 2
Maelezo
Jinsia Kike
Kazi yake Mwanafunzi
Mwimbaji wa taarab
Familia Mzee Kizito
Ndugu Cheusi Kizito
Shoti
Dullah
Matona
Faisaljumla wapo 17
Dini Mwislamu
Utaifa Mtanzania

Sabrina Kizito ni jina la uhusika kutoka katika tamthilia ya Siri ya Mtungi kutoka nchini Tanzania. Uhusika umechezwa na Patricia Nyamaka. Sabrina ni msichana mpole sana, mwenye kutaka kujua mengi ya dunia iliyomzunguka. Mdadisi, na mwingi wa taarifa kuhusu familia yake. Ana mengi aliyosikia, mbali pia kujionea, hasa vituko vya mama yake mkubwa Bi. Farida. Sabrina ni msichana mwenye kipaji cha uimbaji wa taarab ambacho amerithi kutoka kwa mama yake mzazi, Vingawaje. Alianza kuonesha ujuzi na uwezo wake wa kuimba taarab kwenye sehemu ya pili ya msimu wa kwanza. Pamoja na vikwazo vingi kutoka kwa baba yake mzazi, Mzee Kizito, hatimaye akamruhusu kuwa mmoja kati ya wanakundi la taarab. [1]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sabrina Kizito Archived 12 Septemba 2016 at the Wayback Machine. katika wavuti rasmi ya Siri ya Mtungi.