Siri ya Mtungi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Programu ya mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins (JHUCCP)

Siri ya Mtungi ni tamthilia ya televisheni kutoka nchini Tanzania.

Imetayarishwa na Media for Development International (MFDI), waliopewa jukumu na Programu ya mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins (JHUCCP) Tanzania kwa msaada wa watu wa Marekani kupitia USAID.[1]

Ilipozinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2012, imekuwa tamasha maarufu zaidi la televisheni nchini Tanzania na nchi nyingine zinazozungumza Kiswahili.[2] Tamthilia hiyo inawaleta pamoja wasanii bora wa Tanzania, waandishi, wanamitindo wa nguo, wakurugenzi wa sanaa, waigizaji na watendaji wa filamu kwenye mafanikio makubwa ya ukuaji wa tasnia ya filamu na televisheni Tanzania.[3]

Uamuzi wa kutayarisha tamthilia ya kiwango cha juu inayoongea moja kwa moja na watu wa Tanzania na Afrika Mashariki, ulileta mapinduzi katika mtandao wa afya ya Mtazania.[1]

Kwenye hii tamthilia ya televisheni, wahusika wanakabiliwa na masuala yanayotoa changamoto kwa Watanzania wote.[1] Changamoto hizo ni pamoja na matatizo ya afya, uzazi wa mpango, kondomu, VVU/UKIMWI, matumizi ya dawa za kulevya, na kadhalika.[1][4]

Inazungumzia masuala ya kitamaduni kwa mfano ndoa za mitala, uaminifu, umaskini, familia, na mahusiano ya kimapenzi.[1][4] Wahusika wanataka kujua namna ya kuyafanya maisha yao kuwa bora; mara nyingine wanaweza, wakati mwingine wanashindwa au hawajui jinsi ya kufanya. [1][2]

Maelezo ya jumla[hariri | hariri chanzo]

“Siri ya Mtungi” ni hadithi kuhusu familia kubwa, na wahusika wengi waliobeba uhusika usio wa kawaida. Hadithi hiyo inafuatilia na kuonesha maisha ya Cheche, mpiga picha mwenye ubunifu na umahiri na studio ya kupiga picha ya Mtungi.[1] Hadithi huanza haraka, na watazamaji wanaona kwamba tamthilia ina wanawake wenye mvuto, kama Tula, mpenzi wake Cheche wa shule, na Lulu, mwanamke maarufu.[1][2]

Kwa mfano, Cheche ni mfano wa mwanamume anayejaribu kuwa mume mzuri na baba mwema, lakini ana hatia katika tabia yake. Uhusiano kati yake na mke wake, Cheusi, hufungua mazungumzo kuhusu mpango wa uzazi, ndoa, na uaminifu.[1][2]

Mzee Kizito ni mtu anayeheshimika sana katika jamii ya Bagamoyo.[5] Yeye ana watoto wengi wanaozaliwa na wake zake watatu, Farida, Mwanaidi na Vingawaje.[5] Lakini, hii bado haitoshi, alimpenda pia Nusura, ua la yungiyungi lililochanua katika jamii.[1][5] Kile ambacho hajui ni kwamba Nusura ana VVU; baada ya ujauzito wake Nusura lazima ajifunze kuishi kama mama mwenye VVU.[5]

Hadithi na Afya[hariri | hariri chanzo]

Mpango wa uzazi unaonyeshwa kama ufunguo wa afya na maendeleo ya jamii.[5] Ila, kwa kawaida, mwanamke hawezi kujadili na mume wake kwa urahisi kuhusu uzazi wa mpango.[5] "Siri ya Mtungi” inatumia ucheshi na mchezo kwa kuanzisha mada hiyo.[6]

Katika Tanzania na Afrika Mashariki, kuna unyanyapaa sana kwa watu wanaoishi na VVU.[6] Katika “Siri ya Mtungi” Nusura ni msichana mzuri, mwenye akili na anayeheshimika, lakini alipata maambukizi ya VVU.[1] Mtu yeyote anaweza kuwa na VVU. Anaweza kuwa si kahaba au mtu ambaye ni mzinzi.[6]

Mkurugenzi wa tamthilia, John Riber, alisema: “Ni kweli tunatengeneza sinema kuhusu maendeleo. Lakini hatuhubiri au kutoa majibu. Masuala katika maisha yetu yamechanganyika. Hakuna majibu rahisi. Na hayo ndiyo yanayounda tamthilia."[1] “Hatuwezi kutoa maamuzi rahisi. Lakini tunaweza kutoa hadithi zinazoleta matumaini, zinazoonyesha kwamba watu hawako peke yao wanapokabili changamoto. Tamthilia hii ya televisheni inapenya ndani ya milango iliyofungwa. Tunaona na kusikia mambo nyeti juu ya mahusiano.”[1]

Siri ya Mtungi inavunja kanuni za kijamii, vikwazo vya kitamaduni, na inazungumzia wazi mada za afya.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 Siri ya Mtungi - Made for Television, Made for Tanzania (en-GB). www.siriyamtungi.com. Iliwekwa mnamo 2019-07-25.
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 Siri ya Mtungi, retrieved 2019-07-25 
  3. Michuzi Blog. Tamthilia ya "SIRI YA MTUNGI" yazinduliwa rasmi leo. MICHUZI BLOG. Iliwekwa mnamo 2019-07-25.
  4. 4.0 4.1 About | K4Health. www.k4health.org. Iliwekwa mnamo 2019-07-25.
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 5.5 Family Planning: Conversation Guide (PDF in Swahili). FHI 360. Iliwekwa mnamo 2019-07-25.
  6. 6.0 6.1 6.2 About | K4Health. www.k4health.org. Iliwekwa mnamo 2019-07-25.
Video-x-generic.svg Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Siri ya Mtungi kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.