Nenda kwa yaliyomo

Steven (Siri ya Mtungi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Steven
muhusika wa Siri ya Mtungi

Taswira ya Steven (Siri ya Mtungi) (uhusika umechezwa na Yoeri Mpira)
Imebuniwa na MFDI Tanzania
Imechezwa na Yoeri Mpira
Idadi ya sehemu 26
Misimu
1, 2
Maelezo
Jinsia Kiume
Kazi yake Mwanafunzi, rapa wa muda
Ndugu Duma
Dini Mkristo
Utaifa Mtanzania

Steven ni jina la uhusika kutoka katika tamthilia ya Siri ya Mtungi kutoka nchini Tanzania. Uhusika umechezwa na Yoeri Mpira. Maisha yake ni tabu karibia kila siku. Makuzi ya kuishi geto na kaka yake, bado elimu na mazingira ya uhuni yanayomzunguka. Hana la kujifunza kutoka kwa kaka yake isipokuwa juhudi anazofanya ili mdogo wake apate maisha mazuri. Steven ni kijana mwenye kipaji cha kurap (jina la kisanii ni Dogo-D) na mzuri katika somo la hesabu.

Mwepesi kuiga mambo yasiyo na maana, mfano umalaya alijaribu kufuata nyayo za kaka yake Duma, lakini ukali wa kaka yake ulisababisha aachane na tabia za kaka yake. Kijana mwenye nidhamu na asiyependa kulumbana. Hawezi hata kujitetea katika mambo mengi sana. Mara nyingi hutegemea wakati useme badala ya kusema ili ijulikane. Ni mmoja kati ya wahusika wanaoishi maisha ya dhiki mno. Maisha ya geto yamejawa na mikasa na manyanyaso mbalimbali. [1] Katikati mwa msimu wa pili, anapata ufadhili wa kuishi nyumbani kwa mwalimu wa somo la hesabu hadi hapo Duma atakaporudi safari yake ambayo hasa mwenyewe aliita ya matumaini na maisha mapya.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Steven (Siri ya Mtungi) Ilihifadhiwa 12 Septemba 2016 kwenye Wayback Machine. katika wavuti rasmi ya Siri ya Mtungi.